Ni Hospitali gani ya Umma (ya Serikali) hasa hasa Mkoani Dar es Salaam yenye Huduma Rafiki ya Kung'oa Meno?

Nenda muhimbili hutajutia ila inabidi uwahi sana asubuhi kuepuka foleni. Hakuna kuhonga wala takrima
 
Kuna wakati mnazi mmoja hospital ilikua bora sana kwenye kitengo cha meno na macho.
....hata sasa bado wako vizuri. Utoaji, meno bandia na usafi wa kinywa MM wanajitahidi sana na kwa gharama nafuu
 
....hata sasa bado wako vizuri. Utoaji, meno bandia na usafi wa kinywa MM wanajitahidi sana na kwa gharama nafuu
Nashukuru kujua hilo sijaenda pale kama miaka 6 ila ilikua bora sana
 
Mkuu, mnazi mmoja wapo vizuri sana. Na mbagala kipati ya binafsi lkn, inaitwa sabrina ipo poa pia.
 
Nenda pugu pale pugu shule ya msingi Kuna hospital ya serikali cjui zahanati nilingoa jino pale anangoa vzr Sana yaani kesho yake unakula kbsa chakula
I'll kwenye swala maumivu wakati wa kungoa hariepukiki Ila mizizi yote jino lote analitoa
 
Naomba kupata mrejesho wa yeyote aliyewahi kwenda SD Dental Clinic international, Dar es Salaam.
 
Kuna wakati mnazi mmoja hospital ilikua bora sana kwenye kitengo cha meno na macho.
Mnazi mmoja nilinusurika kufa ******* walikua sijui na ganzi feki mbwa wale?ila nashukuru Mungu nlifanikiwa kukimbia
 
Vp kuhusu kairuki ipo vizuri kwenye huduma ya meno? Ambaye amepitia hapo atupe mrejesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…