brokenagges
Member
- Sep 29, 2022
- 58
- 33
Hii ni dharau kwa Rais samia pamoja na serikali yake kwa ujumla.
Ni jambo lenye fedheha kabisa rais anapotoa maelekezo yasizingatiwe. Mkuu wa nchi anapoongea inakuwa ni amri. tumekosa mvua kwa muda mrefu na kumekuwepo na uhamasishaji kutoka kwa mheshimiwa Rais, makamu wa rais, waziri mkuu na hata mawaziri tamisemi na mazingira tukihamasishwa kuotesha miti mipya pamoja na kuitunza miti ambayo imeshaoteshwa.
Viongozi wamekuwa wanakemea kwa ukali kabisa ukataji miti hovyo, lakini hali ni tofauti kwenye ngazi za kusimamia utekelezaji wa maagizo ya mheshimiwa Rais hii imetokea leo mkoani Arusha.
Inavyoonekana ni kwamba waharibifu wanavizia siku ambayo ni sikukuu kama leo sikukuu ya UHURU wa TANGANYIKA maana ya kwamba ofisi za serikali zimefungwa ndipo wanapofanya huu uharibifu watu wanakata miti hovyo na vibali wanasema wanavyo.
Nilikuwa naongea na anayesimamia kukata miti hii leo ambaye anatarajia kufungua mgahawa mbele ya jengo la ushirika (ARCU) sehemu ambayo miti imekatwa akaniambia inafanyika hivyo kwa sababu inazuwia biashara zilizopo mbele ya hilo jengo hazionekani vizuri,
nikajiuliza ni nani hao ambao wanatoa vibali vya kukata miti kwa sababu za kipuuzi namna hii?
Kwa sababu tu ya posho ndo inawapa watu wahusika kujiondoa ufahamu kiasi hicho?
Pamoja na kukemea kote kwa Rais na serikali yake kuhusu swala la uhifadhi wa mazingira watu hawaogopi wala hawajali.
Waliotangulia waliotesha hiyo miti wakiamini kwamba ingetengeneza madhari nzuri katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuhifadhi mazingira na kutengeneza kivuli na upepo mzuri ikiwa inaongeza uzuri na muonekano wa kijani.
Nimuombe Mkuu wa mkoa wa Arusha na ambaye ni mwakilishi namba moja wa Rais kwa ngazi ya mkoa afuatilie hili swala kwa umakini atabaini upumbavu unaofanyika na watendaji katika ofisi ambayo wapo waliopoteza uaminifu ili aweze kuwachukulia hatua wahusika na hasa waliotoa kibali na hata walioshawishi hadi kutolewa kwa kibali cha ukataji huu ambao ni ubaribifu.
Ukataji wa miti limekuwa ni jambo la kawaida sana hasa ktk mkoa huu ambao ulipendezeshwa kwa ukijani wa miti sehemu nyingi pembezoni ni mwa barabara lakini imeonekana kila inapojitokeza kufunguliwa biashara hasa za maduka ama migahawa kwenye nyumba zilizopo pembezoni mwa barabara basi wahusika hukata miti wakiamini kwamba itaacha biashara zao zionekane. Na ajabu ni kwamba pembeni ya hizi biashara na ndani ya jengo hili kwa upande mwingine imekuwepo tawi la Bank ya BOA ambalo limekuwa likiendeshwa miaka mingi bila ya kukata miti lakini zimekuja hizi biashara za mgahawa na duka ndipo ukataji huu unajitokeza.
Serikali isipochukua hatua kwenye hili hii itakuwa ni hatari na mji unaenda kuwa jangwa.