Dialogist
JF-Expert Member
- Apr 14, 2014
- 1,167
- 1,872
Wandugu Habarini...
Nimepata Tashtwiti Ya Kuandika Leo Juu Ya Humphrey Polepole Baada Ya Kutafakari Kwa Kina.
Ni Wazi Hakuna Mpenzi Wa Siasa Za Tanzania Asiyemjua Huyu Jamaa. Naweza Sema Kwa Namna Moja Au Nyingine Alikua Nyota Ya Mchezo Sana Katika Kubadilisha Siasa Za Nchi Hii Kipindi Cha Magufuli Na Hata Baada Ya Magufuli, Miaka Ya Mwanzoni Ya Uongozi Wa Samia (Mh.).
Humphrey Polepole Mara Zote Amejitanabaisha Kama Miongoni Mwa Wazalendo Wa Kweli Wachache Sana Wa Taifa Hili Kwa Haiba, Mwonekano Na Maneno Yao. Bahati Mbaya Baada Ya Mama Kuingia Madarakani Akaona Anafaa Zaidi Kutuwakilisha Nje, Kutokana Na Uwezo Wake Basi Akaonekana Anaweza Kuisaidia Nchi Vizuri Zaidi Akiwa Balozi Kuliko Kubaki Hapa Nchini. Pamoja Na Hilo Bado Tumeona Mara kadhaa Akiendelea Kupambana Huko Huko Kuhakikisha Kupitia Yeye Na Mahusiano Yetu Na Nchi Anazotuwakilisha, Basi Nchi Yetu Ipate Kufaidika Na Matokeo Hayo. Lakini Bahati Mbaya Juhudi Zake Sidhani Kama Zinazaa Matunda. Sidhani Kama Anaonekana Ni Msaada Wowote Akiwa Nje, Kwa Fikra Zangu Binafsi.
Kwa Muktadha Huo, Nawashauri CCM Huyu Mtu Ni Wakati Wa Kumrejesha Nchini Na Kumpa Nafasi Ndani Ya Chama. Ni Mtu Huyu Pekee Atakayeikomboa CCM Iwapo Upande Wa Wapinzani Wao Chadema Wataamua Kumchagua TUNDU LISSU Kua Mwenyekiti Wao. Haiba Ya POLEPOLE na Ya LISSU Kwenye Maono Juu Ya Taifa Letu Vinafanana Na Wananchi Wanawapenda Sana Na Kuwaamini. Hivyo Tashtwiti Yangu Imeona Ni Heri Atoke Huko Nje Arudi Nchini.
Wanachama Wa Chama Cha Mapinduzi Na Viongozi Wao Fuateni Ushauri Huu.
Nachelea Kusema HUMPHREY POLEPOLE ndio Mkombozi Sahihi Wa CCM kwa Sasa.
Karibuni Kwa Mjadala