Ni huzuni, nimeachana na mke wangu kisa tatizo la kukoroma usiku

Tengana vyumba kama hamna sababu ya kuwa pamoja.
 
Hulipendi kivipi kwani huwa unajisikia ukoromapo? Ukioa tena au shem akirudi kila mtu awe na chumba chake cha kulala, siku za mech mnapiga popote zen kila mtu anapotelea geton mwake simu mnazo, ukitaka tena piga simu aje au uende.

Jitahidi usiwe unachoka sana, uchovu mwingi huleta ukoromaj vilevile pendelea kulalia tumbo au ubavu na si kulalia mgongo
 
Mwanaume akilala na mwanamke Hadi kukoroma ni kwamba ana Amani kuwa Yuko na MTU Sahihi na Salama, sasa hiki kizazi cha Nyoka ndio kigumu kuelewa
 
Fanya mazoezi punguza unene, acha pombe, tafuta ile mitungi ya kupumulia ukilala, kafanye upasuaji wa kupunguza nyama kwenye njia ya hewa.
 
Ni muhimu kwanza ujue historia yako. Je ulikuwa unakoroma tangu ukiwa mtoto? Mfano je una nyama za puani? Je wewe ni mnene na una uzito uliopitiliza???? Ila all in all, huyo mwanamke kuondoka ni haki yake, hakuna anayeweza kuvumilia matatizo. Suluhisho kuna mito ipo madukani unaweza kununua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…