Ni ipi dawa ya kurudisha mn'gao wa rangi ya nguo, au kuzuia nguo isipauke hasa nyeusi?

Ni ipi dawa ya kurudisha mn'gao wa rangi ya nguo, au kuzuia nguo isipauke hasa nyeusi?

Uhakika Bro

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2022
Posts
3,644
Reaction score
4,315
Wataalamu na wasomi na wajuzi hivi kwa bongo hizi dawa zipo.

Watafiti tunaomba dawa ya kurudisha nguo ziwe mpya maana nakumbuka zamani tulivaa nguo hadi ichanike, ila sasa hivi hata ikipauka tu tayari inaonekana chakavu hata kama bado haijaqualify kuwa dekio jipya. Sasa si wengine tunataka ikiisha iishe kweli beyond reasonable doubt sio kimaigizo maigizo.

Ukizingatia nyingine hasa hizi nyeusi zina kiherehere sana cha kupauka kabla hujaichoka hata. Unakuta ukivaa juu na chini vyeusi; basi moja inamuaibisha mwenzie ukilinganisha inakuwa 'sio nyeusi kiviiile😏'. Mambele wanazo brand za kufanya hiyo kazi je bongo zipo?

Kuna mtu mmoja akaniambia ichukue ikunje vizuri iweke kabatini mda mrefu ukiitoa unakuta mpyaaa 😂😂😂😂🤦‍♂️. Achana na huyu jamaa naomba mwenye suluhisho halisi aokoe jahazi basi.
 
Nguo ikipauka weka pembeni nunua nyingine acha maneno ming 🤣🤣😃😃
Ujasiriamali tu, we hutaki kuanza kuvaa mitumba mipya ya nguo zako mwenyewe?
 
Za kizungu;
1657091080338.png
 
Back
Top Bottom