Ni ipi hatima ya Haji Manara endapo akienguliwa Yanga?

Ni ipi hatima ya Haji Manara endapo akienguliwa Yanga?

Kwa anaejua mahala huyu boya anaweza enda baada ya kufurushwa huko alikojibanza kwa kimvuli cha usemaji wa timu
Manara ni bonge la msanii!! Atalia kisanii machozi debe na kumwangukia Mo!! Mwisho wa siku simba watasema mwana mpotevu hakataliwi kurudi nyumbani na mwanao akikunyea hauukati mkono.

Ila ukweli ni kwamba Manara ni mganga njaa!! Popote penye riziki atakaa!! Hana mapenzi na Simba wala Yanga!! Ana mapenzi na pesa za Simba na Yanga!! Hapo alipo anawang'ong'a Yanga, laiti wangelijua!! Wakifungwa anachekea tumboni, akielemewa anaenda kuchekea chooni!
 
Wanayanga hawanaga uvumilivu.
Natabiri Kocha Nabi na Haji watatimuliwa Yanga kisha Haji atarudi kuwaomba msamaha Simba.

Atasema kule Yanga alienda kufanyakazi baada ya kuachishwa kazi Simba, Yeye hajawahi kuwa mwanayanga.

Atatoa kadi yake ya uanachama ya Simba ataiweka mezani, atajikwaruza mwilini hadi itatoka damu, kisha atasema si mnaona hadi damu yangu inarangi nyekundu? - mimi ni Simba damu, sijawahi kuwa Uto.

Atasema akiwa kule Yanga alikuwa anatoa siri nyingi za kambi ya Yanga na kuisaidia Simba kuja kutwaa ubingwa

Kisha atasema kule uto mwenye akili ni Baba yake na Mzee Kikwete tu!. Waliobaki wote ni kama vile hamnazo!.

Huyu ndio Haji ninaemfahamu.
 
Kwa anaejua mahala huyu boya anaweza enda baada ya kufurushwa huko alikojibanza kwa kimvuli cha usemaji wa timu
Sijawahi kumkubali Manara na haitotokea iwe hivyo, lakini kwenye swala la riziki mtowaji ni Mungu na hakuna ajuwaye kesho.

Mchukie mtu kwa kiasi usiingilie mpaka kazi ya Mungu alichotuandalia binadamu.
 
Naskia amesomea propaganda huko Taiwan sasa usishangae wajomba wa mataifa huko wakahitaji huduma yake😁😁😁🐸
 
Kwann aenguliwe??

Manara ndio anacheza??


Alipokua Simba, mpaka tunapigwa goli tano tanoo ..ilikuaje????


ACHENI KUA MIROHO MIBAYA YAKIJINGA JINGA.

MANARA HIYO NISEHEM YA MAISHA YAKE, RIDHIKI YAKE.
 
Kwann aenguliwe??

Manara ndio anacheza??


Alipokua Simba, mpaka tunapigwa goli tano tanoo ..ilikuaje????


ACHENI KUA MIROHO MIBAYA YAKIJINGA JINGA.

MANARA HIYO NISEHEM YA MAISHA YAKE, RIDHIKI YAKE.
Wamesahau Manara ni kada wa chama la wana, ikimpendeza Chief Hangaya usishangae siku unaambiwa Manara ndio mkurugenzi wa mawasiliano ikulu au ndio msemaji wa wizara ya michezo.
 
Kwasababu tabia ya uchumia tumbo ipo ndani ya DNA ya CCM ataenda nyumbani kwao kwenye kijani
 
Back
Top Bottom