Wanayanga hawanaga uvumilivu.
Natabiri Kocha Nabi na Haji watatimuliwa Yanga kisha Haji atarudi kuwaomba msamaha Simba.
Atasema kule Yanga alienda kufanyakazi baada ya kuachishwa kazi Simba, Yeye hajawahi kuwa mwanayanga.
Atatoa kadi yake ya uanachama ya Simba ataiweka mezani, atajikwaruza mwilini hadi itatoka damu, kisha atasema si mnaona hadi damu yangu inarangi nyekundu? - mimi ni Simba damu, sijawahi kuwa Uto.
Atasema akiwa kule Yanga alikuwa anatoa siri nyingi za kambi ya Yanga na kuisaidia Simba kuja kutwaa ubingwa
Kisha atasema kule uto mwenye akili ni Baba yake na Mzee Kikwete tu!. Waliobaki wote ni kama vile hamnazo!.
Huyu ndio Haji ninaemfahamu.