getrusa
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 2,150
- 1,822
Wakuu nimeona taarifa za kuuwawa kwa mmoja kati ya maofisa wa polisi Uganda
Jambo hili limenipa tafakuri kidogo kutaka kujua historia ya kiutawala ama kiuongozi ya Uganda tangu kupata kwao uhuru.
Siyajui mengi lakini kwa kile kidogo ninachofahamu Uganda imepita katika machafuko kadhaa kabla ya Museveni aliyepo sasa, na bila shaka kuna hatua ya kijamii, na kisiasa zilizopigwa baada ya uongozi wa Museveni.
Swali langu hao wanaotaka Mseveni Kaguta aondoke madarakani lengo lao kubwa hasa ni lipi?, hawafurahishwi na maendeleo ya kiuchumi ya Nchi yao? Ama hawaridhishwi na amani iliyopo kwao mpaka sasa?
Ukiangalia tukio zima la Bob wine, na kundi lake peoples Power unapata shida kujua alie nyuma ya wimbi hili, sidhani kama Bob anaweza kuwa Rais wa Uganda.na akafanya vema kama afanyavyo Museveni sasa bila shaka anatumika je anatumiwa na nani kwa faida ya nani?, juzi kilikuwa na taarifa kuwa atahudhuria kwenye baraza la wawakili Marekani, (nikosolewe endapo siko sawa)
Je, Wamarekani wanaijua zaidi demokrasia ya Uganda kuliko waganda wenyewe? Ama waingereza wanaijua Uganda zaidi kuliko Waganda wenyewe?
Tukio la kuuwawa kwa Mkuu wa polisi nadhani ni Mchezo wa kisiasa wenye lengo la kumwagia mafuta kwenye moto unaoanza kuwaka ili uwake zaidi, sidhani kama serikali wangetaka kumnyamazisha Afisa huyo ilikuwa lazima wamuue yamkini hii ni mbinu ya kisiasa ya kupata wafuasi wengi zaidi ya kuipinga serikali.
Ninapohitimisha ni vema tukakumbuka kiwa Uganda wamegundua mafuta, wanatarajia kuanza kuyachimba Msimamo wa Mh Yower Kaguta Mseveni juu Ya mali hizi za Waganda kwa makampuni ya kibepari ya Ulaya ni wazi, sitarajii waiache nchi hii salama.
Walichokifanya kwa Muamar Ghadafi wa Libya kila mmoja anakifahamu, wanachokifanya Syria Kila mtu anajua walichokifanya Iraq kiko wazi sana.
Sasa wanaelekea Uganda in the name of Demokrasia, wakisha ivuruga Uganda wataacha wakimbizi kwenye Nchi za Afrika Mashariki kisha wao wataendelea kujibebea mafuta kiulaini bila shida.
Biblia inasema
"nitampiga Mchungaji na kondoo watatawanyika"
Kila la heri Uganda ila mkumbuke historia huwa ina kawaida ya kujirudia.