Ni ipi historia ya Uganda?

Ni ipi historia ya Uganda?

getrusa

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
2,150
Reaction score
1,822
Wakuu nimeona taarifa za kuuwawa kwa mmoja kati ya maofisa wa polisi Uganda

Jambo hili limenipa tafakuri kidogo kutaka kujua historia ya kiutawala ama kiuongozi ya Uganda tangu kupata kwao uhuru.

Siyajui mengi lakini kwa kile kidogo ninachofahamu Uganda imepita katika machafuko kadhaa kabla ya Museveni aliyepo sasa, na bila shaka kuna hatua ya kijamii, na kisiasa zilizopigwa baada ya uongozi wa Museveni.

Swali langu hao wanaotaka Mseveni Kaguta aondoke madarakani lengo lao kubwa hasa ni lipi?, hawafurahishwi na maendeleo ya kiuchumi ya Nchi yao? Ama hawaridhishwi na amani iliyopo kwao mpaka sasa?

Ukiangalia tukio zima la Bob wine, na kundi lake peoples Power unapata shida kujua alie nyuma ya wimbi hili, sidhani kama Bob anaweza kuwa Rais wa Uganda.na akafanya vema kama afanyavyo Museveni sasa bila shaka anatumika je anatumiwa na nani kwa faida ya nani?, juzi kilikuwa na taarifa kuwa atahudhuria kwenye baraza la wawakili Marekani, (nikosolewe endapo siko sawa)

Je, Wamarekani wanaijua zaidi demokrasia ya Uganda kuliko waganda wenyewe? Ama waingereza wanaijua Uganda zaidi kuliko Waganda wenyewe?

Tukio la kuuwawa kwa Mkuu wa polisi nadhani ni Mchezo wa kisiasa wenye lengo la kumwagia mafuta kwenye moto unaoanza kuwaka ili uwake zaidi, sidhani kama serikali wangetaka kumnyamazisha Afisa huyo ilikuwa lazima wamuue yamkini hii ni mbinu ya kisiasa ya kupata wafuasi wengi zaidi ya kuipinga serikali.

Ninapohitimisha ni vema tukakumbuka kiwa Uganda wamegundua mafuta, wanatarajia kuanza kuyachimba Msimamo wa Mh Yower Kaguta Mseveni juu Ya mali hizi za Waganda kwa makampuni ya kibepari ya Ulaya ni wazi, sitarajii waiache nchi hii salama.

Walichokifanya kwa Muamar Ghadafi wa Libya kila mmoja anakifahamu, wanachokifanya Syria Kila mtu anajua walichokifanya Iraq kiko wazi sana.

Sasa wanaelekea Uganda in the name of Demokrasia, wakisha ivuruga Uganda wataacha wakimbizi kwenye Nchi za Afrika Mashariki kisha wao wataendelea kujibebea mafuta kiulaini bila shida.

Biblia inasema

"nitampiga Mchungaji na kondoo watatawanyika"

Kila la heri Uganda ila mkumbuke historia huwa ina kawaida ya kujirudia.
 
Huyo mseveni kwani duniani alizaliwa peke yake kuwa kiongozi wa Uganda kwa sababu tu kwenye uongozi wake kuna Amani na Akifa je what next?
 
Sidhani kama Museveni anafanya vibaya,shida ninayoiona hapo kwa waganda ni kuwa wanahitaji ideas mpya,raisi Museveni inabidi aamini kuwa kuna watu wengine zaidi yake yeye wanaoweza kuiendesha Uganda,kwani unafikiri JK alivyoachia kijiti kwa JPM,au Obama alivyomuachia Trump ilikuwa uwezo wake wa kuongoza nchi umeisha!

Ni lazima tu ukubali kuwa wako wengine wanaoweza kufanya mabadiliko tena hata zaidi yako, ung'ang'anizi wa madara umezigharimu nchi nyingi,kwani inafikia mahali wananchi hawakuhitaji tena wanataka mtu mwingine ili aweze kuwaletea mabadiliko wanayoyahitaji
 
Huyo mseveni kwani duniani alizaliwa peke yake kuwa kiongozi wa Uganda kwa sababu tu kwenye uongozi wake kuna Amani na Akifa je what next?
Ni jambo jema kuonja sumu, endapo hujui inauaje.

Uongozi wa Milton Obote ulikuwaje?

Uongozi wa Yusuf Rule ulileta kipi kwa waganda?, Uongozi Wa Iddih Amini Uliletaa mapinduzi yapi kiuchumi na kijamii..?

Je, Mh Yoweri Kaguta Mseveni ali rithi maendeleo yapi kiuchumi, kijamii ambayo ameyaharibu kwa uongozi wake kisiasa?
Je, hana maono Kwa Taifa?

Hao mnaotaka waongoze Uganda mwadhani waweza kuwa na vision ileile aliyo nayo Mseveni?

Demokrasia ni wendawazimu ni vema tukajifunza kwa waliopata madhara ya kukumbatia mbinu na mikakati ya Ulaya kudhoofisha nchi zetu, wivu kuwa fulani kakaa madarakani muda mrefu yampasa aondoke haikufanyi wewe kuwa kama yeye.

Endapo akifariki hilo ni jambo jingine na huenda likawa na majibu yake kwa wakati huo..
 
Ni jambo jema kuonja sumu, endapo hujui inauaje.uongozi wa Milton Obote ulikuwaje?
Uongozi wa Yusuf lule ulileta kipi kwa waganda?, Uongozi Wa Iddih Amini Uliletaa mapinduzi yapi kiuchumi na kijamii..?

Je, Mh Yoweri Kaguta Mseveni aliridhi maendeleo yapi kiuchumi, kijamii ambayo ameyaharibu kwa uongozi wake kisiasa?
Je hana maono Kwa Taifa?
Hao mnaotaka waongoze Uganda mwadhani waweza kuwa na vision ileile aliyo nayo Mseveni?

Demokrasia ni wendawazimu ni vema tukajifunza kwa waliopata madhara ya kukumbatia mbinu na mikakati ya Ulaya kudhoofisha nchi zetu, wivu kuwa fulani kakaa madarakani muda mrefu yampasa aondoke haikufanyi wewe kuwa kama yeye.
Endapo akifariki hilo ni jambo jingine na huenda likawa na majibu yake kwa wakati huo..
Nijibu swali na Akifa je itakuwaje? Ina maana Uganda itarudi kule kule ilikotokea Kwa nini sasa kwenye utawala wake asijitahidi kuweka demokrasia au mfumo ulio imara ata kama ikitokea asipokuwepo kesho kuna ambao wataendeleza pale alipoishia.
 
Sidhani kama Museveni anafanya vibaya,shida ninayoiona hapo kwa waganda ni kuwa wanahitaji ideas mpya,raisi Museveni inabidi aamini kuwa kuna watu wengine zaidi yake yeye wanaoweza kuiendesha Uganda,kwani unafikiri JK alivyoachia kijiti kwa JPM,au Obama alivyomuachia Trump ilikuwa uwezo wake wa kuongoza nchi umeisha! ni lazima tu ukubali kuwa wako wengine wanaoweza kufanya mabadiliko tena hata zaidi yako,ung'ang'anizi wa madara umezigharimu nchi nyingi,kwani inafikia mahali wananchi hawakuhitaji tena wanataka mtu mwingine ili aweze kuwaletea mabadiliko wanayoyahitaji...
Mkuu umesema vema lakini ninachokiona kwa uzoefu wangu kubadiri uongozi ni sawa na kucheza santakarawe.

Sisi pia Tanzania limetuathiri sana jambo hili tukidhani tunasifiwa kumbe tunajiharibu mathalani yaliyoachwa Mwl Nyerere, na mawazo yake hayakuweza kudumu wakati wa Mh Mwinyi, alipokuja Mkapa ya Mwinyi yakaishia hapo.. tukaenda vema kiasi fulani kama Taifa alipokuja kikwete akafanya yake, leo hii Taifa linamkumbuka Nyerere, kwa viwanda na mengi aliyokuwa na maono nayo.!

Hebu angalia Russia Putin amekuwa madarakani kwa muda gani ilipokuwa Russia ndipo leo?
Angalia Ujerumani na Nchi nyingine ambazo viongozi wake wake wadumu kwa muda mrefu.
 
Ninapohitimisha ni vema tukakumbuka kiwa Uganda wamegundua mafuta, wanatarajia kuanza kuyachimba Msimamo wa Mh Yower Kaguta Mseveni juu Ya mali hizi za Waganda kwa makampuni ya kibepari ya Ulaya ni wazi, sitarajii waiache nchi hii salama.
Mkuu hapo hapo angalia Nigeria mafuta yalipogunduliwa tukasikia na vita ya Biafra imeanza.
 
Usiwasingizie wazungu , hawajamtuma mseveni aue watu hovyo wala kuua demokrasia nchini kwake, mshauri afuate katiba.
 
Usiwasingizie wazungu , hawajamtuma mseveni aue watu hovyo wala kuua demokrasia nchini kwake, mshauri afuate katiba.
Una hakika? aliyeua na aneua Libya leo ni Muamar Ghadafi? Anayeua Syria ni Assad,!? Au anaeua na aliyuruga Iraq ni Sadam Hussein? Machafuko ya Nigeria baada ya mafuta je yalisababishwa na Wanaigeria?

Ukiwa na maswali hayo kichwani utaondoa tongo tongo machoni.. usiwe shabiki wa usilolijua kirakachopata shida sio wewe ni wajao baada yako.
 
Ni jambo jema kuonja sumu, endapo hujui inauaje.
Uongozi wa Milton Obote ulikuwaje?
Uongozi wa Yusuf Rule ulileta kipi kwa waganda?, Uongozi Wa Iddih Amini Uliletaa mapinduzi yapi kiuchumi na kijamii..?

Je, Mh Yoweri Kaguta Mseveni ali rithi maendeleo yapi kiuchumi, kijamii ambayo ameyaharibu kwa uongozi wake kisiasa?
Je, hana maono Kwa Taifa?
Hao mnaotaka waongoze Uganda mwadhani waweza kuwa na vision ileile aliyo nayo Mseveni?

Demokrasia ni wendawazimu ni vema tukajifunza kwa waliopata madhara ya kukumbatia mbinu na mikakati ya Ulaya kudhoofisha nchi zetu, wivu kuwa fulani kakaa madarakani muda mrefu yampasa aondoke haikufanyi wewe kuwa kama yeye.
Endapo akifariki hilo ni jambo jingine na huenda likawa na majibu yake kwa wakati huo..
Najua una ujumbe unataka kutupatia.
Umekosa sifa moja tu,huyo Mzee Yowel aanze kuamini kuwa uganda ni ya waganda sio yake.

Kingine tabia ya kudhani bila yeye maendeleo hayaji ni upuuzi fulani hivi.

Kama watu wa uganda wataanza kutumika, ni kosa la watawala kutoamini kuwa kuna wenye mawazo mbadala na kutotaka kuwapa wengine nafasi.
 
Chad walipogundua mafuta ndipo vita vya wenyewe kwa wenyewe vikaanza na baadae Libya ikaivamia Chad lakini Ghadafi alichapwa vibaya.
 
Watu kama hao wakishaonjeshwa pipi ni vigumu kutema hata mate mpaka iishe utamu ndo anaweza kutema mate!!!!
 
Huyo M7 miaka zaidi ya thelathini madarakani, wewe mtoa uzi unaona no sawa??
 
Najua una ujumbe unataka kutupatia.
Umekosa sifa moja tu,huyo Mzee Yowel aanze kuamini kuwa uganda ni ya waganda sio yake.

Kingine tabia ya kudhani bila yeye maendeleo hayaji ni upuuzi fulani hivi.

Kama watu wa uganda wataanza kutumika, ni kosa la watawala kutoamini kuwa kuna wenye mawazo mbadala na kutotaka kuwapa wengine nafasi.
Kama ni ya Waganda Je Yowel Kaguta Museveni yeye sio Mganda? Au hao waganda uwasemao wewe ni wepi?

Kati ya hao Waganda waliokuwa wanacheza densi na kula bata wakati yeye akiwa msituni na askari wako miaka ya 80 nani hasa ni Mganda..?
 
Nijibu swali na Akifa je itakuwaje? Ina maana Uganda itarudi kule kule ilikotokea Kwa nini sasa kwenye utawala wake asijitahidi kuweka demokrasia au mfumo ulio imara ata kama ikitokea asipokuwepo kesho kuna ambao wataendeleza pale alipoishia.
Huyu jamaa atakuwa mmoja wa wanafamilia wa Mu7, juzi hapa katoka kuweka saini mikataba China. Yaani wawakilishi walikuwa yeye Mu7, mkewe na shemeji yake!!
 
Huyo M7 miaka zaidi ya thelathini madarakani, wewe mtoa uzi unaona no sawa??
Ubaya wake ni upi? Ama huo usio kuwa usawa ni upi? Unafahamu ili kulipitisha Taifa katika hatua moja kwenda nyingine unahitaji miaka mingapi ya kiutawala?
Hebu nambie Puttin yupo madarakani kwa miaka mingapi sasa.?
Kwanini hao Marekani hampigii kelele..?
 
Nijibu swali na Akifa je itakuwaje? Ina maana Uganda itarudi kule kule ilikotokea Kwa nini sasa kwenye utawala wake asijitahidi kuweka demokrasia au mfumo ulio imara ata kama ikitokea asipokuwepo kesho kuna ambao wataendeleza pale alipoishia.
"AJITAHIDI KUWEKA MFUMO IMARA BAADA YAKE "

hiyo ndio hoja ya msingi niliyo iona kwako mkuu. Jitihada anazozifanya huenda anazijua mwenyewe kwani kwa uhakika hakuna aishie milele.
Ila jitihada za kulazimishwa uachie madaraka ili fulani nae atawale nadhani hiyo sio sawa sabbu katika huo ugomvi wa kugombania madaraka ndipo tunapopata mauaji ya watu ambao hawakustahili kufa sabbu tu eti tunataka fulani nae atawale sabbu fulani katawala kwa muda mrefu,!
Kumbukeni wale wanaokufa ama kuuwawa ili kugombea fulani nae atawale au fulani aendelee kutawala, ni wazazi na wanaacha watoto ambao bila shaka hawakustahili kubaki yatima kwa faida tu ya wanasiasa wachache.!
 
Huyu jamaa atakuwa mmoja wa wanafamilia wa Mu7, juzi hapa katoka kuweka saini mikataba China. Yaani wawakilishi walikuwa yeye Mu7, mkewe na shemeji yake!!
Ukiondoa nafasi yake kama mke je Jhanet hana nafasi yoyote serikalini inayompa fursa kuwakilisha taifa katika maamuzi?
Kisiasa au kielimu?
 
Kenya wana mkono kwenye hili la kumsambaratisha museveni ili bomba la mafuta lipite Kenya.
 
Back
Top Bottom