Ni ipi maana halisi ya kumkomboa Mwanamke?

Unaona sasa?
Kama mwanamke hatafundishwa ataona ni haki yake kupigwa, hata watoto wakifanyiwa ukatili hawataona ni vibaya wataona ni haki yao kufanyiwa hivo.

Ndio maana kuna jambo lililetwa humu baba anabaka watoto wake, mama wa watoto alivyogundua hajashitaki popote akaondoka akaachana na mume wake. Kuondoka aliacha watoto , yule baba akaendelea kubaka mtoto na majirani wakajua ila hawakufanya chochote hadi mwisho wa siku mtoto ana ujauzito wa baba ndio unaona wanasema ni jambo la siku nyingi sana, hata mama yao aliamua kuondoka baada ya kugundua hilo.

Sasa hapa utagundua mwanamke anahitaji elimu ya kujitambua na kujua kitendo kibaya kikifanyika anatakiwa asikae kimya apaze sauti hadi apate msaada. Na watoto pia.

Leo hii mtu anakuambia hizi elimu zinapotosha wanawake hazisaidii kitu.
 
Ngoja niingie darasani kwanza. Nikirudi nitakujibu.
 
hahahhahaha wengi sana, wanatutamaniiiiii
Mi kama ni kutamani basi huwa ni kuvua pichu yako tu. Kuushuhudia uumbaji wa mungu ila vinginevyo nawapa pole hao wengine na nachela kusema si wanaume halisi.
 
ni kweli lakini tunaendelea mdogo mdogo na wanaume mkiamua nyie ndo mtatusaidia kwa haraka sanaaaa.
 
"When it comes to reality mwanaume ni anaemiliki penis inayoweza kutungisha mimba anytime"

Sio kweli kwamba penis ndiyo inayotungisha mimba. Hayo ni mwazo ya zama za giza.
Mimba hutungwa pale sperm na yai vinapo fuse pamoja.Hii inaweza kufanywa hata kwenye test tubes kutokana na maendeleo ya sayansi.
Fahamu pia kwamba kuna wanaume wengi wenye penis, wanaweza kufanya sex vizuri na hawana uwezo wa kuzaa.
 
Hyo point lkn Hayo ya kukeketwa kwa wanawake Mara nyingi kunafanyika huko vijijini Na makongamano yanafanyika mjini wale watu wa vijijini Hyo elimu inawafikia VP??????????
 
zipi? za wewe kuogopa utashindwa kumnyanyasa akiweza kujitambua?
yaani na sasa hiv hamna kitu kinarudisha maendeleo ya mwanamke nyuma kama mwanaume mwenye insecurity jaman, mmoja ameoa tu mke wake akapata kazi kwenye NGO ya UN eti anamwambia aache hiyo kazi sababu atamshinda mshahara asubiri apate serikalini ili wafanane, kweli? unaona ni sawa?
 
Sawa hizo ni exceptions na ndio maana zinaitw aartificial ways.
Naturally mwanaume anatambulika kwa kumiliki penis and balls.
 
Hili nakubaliana nalo na kwa sie wajanja tuna namna ya ku deal na hio situation vizuri tu. Ni kuteka account ya mke tu mapema ili asisumbue au kuelekeza hela kwenye miradi yenu binafsi ili zisijazane kwenye account.
 
Hili nakubaliana nalo na kwa sie wajanja tuna namna ya ku deal na hio situation vizuri tu. Ni kuteka account ya mke tu mapema ili asisumbue au kuelekeza hela kwenye miradi yenu binafsi ili zisijazane kwenye account.
exactly na mkikaa vizuri mkashirikiana mtasogea mbele haraka mnoooo, wanawake wala hawezi kwenda kuhonga kirahisi kama mwanaume. lakini kumkatisha tamaa sio sawa au kumwambia aache kazi. kuna siku atamuambia asile sana atanenepa amshinde hahaha
wanaume mjiamini jaman sisi pia tunauwezo mkubwa sana, mke kuwa nazo nyingi ni faida kwa familia sana na sio kweli kuwa uwezo wa mwanamke unakuwa limited na uwezo wa mume wake.
 
Ni faida kama mke sio mbinafsi,.maana wengine akipata kazi nzuri tu ni dharau mwanzo mwisho 😹😹😹 hata kazi hataki tena kufanya atalipa beki 3 hata wawili yeye ni sim na kujiremba tu
 
Hapa kuna kitu naona mnapishana.

Mleta mada na wengine wanaona kuwa kinachofanyika now kwa Ke ni kushindana na wanaume. Ila hali Ke wanajitetea kuwa hawashindani ila wanataka wenzao wajitambue kujua haki zao na kupinga mila kandamizi.

Ila kiuhalisia hata mimi ninachokiona kwenye hizi harakati ni kama ke kutaka kushindana na me. Ndio hapa yanakuja mambo ya 50/50. Sidhani hata mleta mada na wengine kama wanatetea ukatili. Mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi tetea ukatili na kukandamizwa kwa mwanadamu mwingine achilia mbali mwanamke.
Mfano hai alioleta Mtende hasa hayo ndio twataraji kuyaona yakiendelea.
 

Acha uongo wewe mama , Mungu yupo anawaona mnavyopotosha jamii , mbaya wenu sio mwanaume mmeumbwa ni wadhaifu kiasili , udhaifu nyie sasa mnatafsiri kunyanyaswa tafuteni namna bora ya kushughulikia udhaifu kuliko kutwisha lawama wanaume . Mnajaribu kukwepa laana Mungu alishusha kw mwanamke kwamba tamaa zenu zitakuwa juu ya mwanaume kwa kosa la kupokea mashauri ya uongo kutoka kwa ibilisi , ibilisi nyoka shetani alimtumia mwanamke kuharibu future ya mwanaume hata leo shetani bado anawatumia kuharibu future za jamii kwa kusingizio manyanyaso kama bibi wa bibi yenu Hawa alivyodanganywa na nyoka shetani wale matunda waliyokatwa watakuwa na ufahamu kama Mungu na nyinyi shetani anawatumia sas kwa slogan kumkomboa mwanamke na ukandamizaji / unyonge / kumiliki / kutawala mnaendeleza hila za shetani kwa kigezo mwanamke akiwa na uwezo sawa au juu ya mwanaume mtakuwa mmekomesha mfumo dume . Wanawake wapumbavu ndio wanaobomoa ndoa zao na jamii kwa ujumla wanawake wenye hekima wanajenga familia zao na jamii kwa ujumla mifani michache msichukilie ku generalise mwanamke ananyanyaswa ana nyimw haki msolvd issue husika nyie wengine hizo harakati ndip kula yenu mmeziba masikio na kufumbia macho ukweli kulinda ajira zenu.
 
Ni faida kama mke sio mbinafsi,.maana wengine akipata kazi nzuri tu ni dharau mwanzo mwisho 😹😹😹 hata kazi hataki tena kufanya atalipa beki 3 hata wawili yeye ni sim na kujiremba tu
huyo atakua hana akili na akiwa hivyo hata asipokua na hela tabia zake ni hizo hizo.
 
jibu swali acha risala, unaona ni sawa huyo dada aache kazi kisa atamshinda mume mshahara? jibu hapo tu. kama ni dhaifu anaogopa nini kupitwa mshahara na mtu dhaifu?
 
Ni kweli, na hali ni mbaya sana huko vijijini hata hapa mjini watoto wengi wanafanyiwa ukatili and still akina mama wanaogopa kupaza sauti, hili suala linahitaji mjadala mpana ila pia wanaume tunaomba muelewe kwamba suala la kumkomboa mwanamke halibatilishi asili ya mwanamke kwa namna yoyote ile, mwanamke bado atabaki kuwa mke, mama na atatimiza majukumu yake kama inavyokubalika katika jamii na kidini, sema tatizo wakina mama nao wakishaingia kwenye hizi haralati wanataka kuchukua nafasi ya mume au kuwa juu ya mwanaume wanasahau asili yao ndio maana wanaume wengi wanapinga hili swala
 
Asante kwa kuweka sawa, naamini sasa watu wataelewa
 
Ni faida kama mke sio mbinafsi,.maana wengine akipata kazi nzuri tu ni dharau mwanzo mwisho 😹😹😹 hata kazi hataki tena kufanya atalipa beki 3 hata wawili yeye ni sim na kujiremba tu
Sasa hii isifanye uone kwamba wanawake wote wanafanya hivyo wapo baadhi wanafanya hivyo lakini kuna baadhi bado wanasimama kwenye asili yao
 
sijataka kusoma comment za wengine ngoja na mimi niweke mawazo yangu.
juzi nimesoma article BBC inazungumzia jinsi watoto wa kike wanavyoozeshwa kipindi hiki cha COVID kwa sababu hawaendi shule, na imeonekana barani Africa wasichana wengi wanaozeshwa sana kipindi hiki. Mind you hao ni watoto wadogo. Nadhani kimjini mjini hizi harakati za kumkomboa mtoto wa kike inaonekana hazina maana kwa sababu baadhi ya watu wameshatoka kwenye malengo, sasa imekua ni fashion.
Ila tusizibeze zimetutoa mbali sana na bado kuna watoto wanahitaji kukombolewa kutoka kwenye mila potofu hasa hasa kwenye hizi nchi zetu maskini.
 
Sasa hii isifanye uone kwamba wanawake wote wanafanya hivyo wapo baadhi wanafanya hivyo lakini kuna baadhi bado wanasimama kwenye asili yao
kwenye mada kama hizi huwa napenda sana kusoma michango yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…