Al Watani
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 21,237
- 31,811
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
nimepitia kamusi mbili tofauti moja ni ya TUKI iliyo chapwa na Oxford latest version ambayo inasema ngeli ya maiti ni I-ZI lkn pia nimepitia kamusi ya Longhorn inayosema ngeli ya maiti ni A-WA wajuvi njooni mnijuze ni ipi ngeli halisi ya maiti?
Nawakumbusha pia ngeli ya uwanja ni U-ZI kwa maana hiyo wingi wa neno uwanja sio Viwanja.
Naomba turudi kwenye swali la msingi, msaada tafadhari
Unapozungumzia alichokifanya marehemu inakuwa unaongelea kitu alichofanya marehemu kipindi cha uhai wake, hivyo utakuwa unaongelea wakati wa uhai wake hivyo itatumika ngeli ya A-WASasa wajuba kwa mfano marehemu ni A-Wa au I-Zi ??
Kwasabau sio kitu hai
Unaweza kusema marehemu ilikuwa mwizi sana
Uwanja kipande cha ardhi iliyowazi na kitatumiwa kwa kitu fulani na Kiwanja ni kipande cha ardhi, aghlabu kinachotumiwa kwa kujengwa nyumba.
Ngeli ni kundi moja la majina yaliyo na upatanisho mmoja wa kisarufi unaofanana na viambishi vya umoja na wingi ambavyo ama hufanana au kulingana.Kwani ngeli ndo Nini[emoji41]
kelphin kepph
Maiti ni i-zi.
Ngeli ya a-wa, kwa ninavyojua mimi, kwa muktadha huu, ni ngeli inayotumiwa kwa vitu hai.
Kwa mfano. Tunasema meza imepatikana. Hatusemi meza amepatikana. Kwa sababu meza si kitu hai.
Tunasema njia imepatikana. Hatusemi njia amepatikana. Kwa sababu njia si kitu hai.
Tunasema kunguru anaruka. Hatusemi kunguru inaruka. Kwa sababu kunguru ni kitu hai.
Tunasema mtoto amepatikana. Hatusemi mtoto imepatikana. Kwa sababu mtoto ni kitu hai.
Inawezekana tunasema maiti amepatikana katika namna moja ya kuisitiri maiti, tunamuongelea mtu aliyefariki kama mzima, kwa kutumia tafsida ya heshima pekee kwa mtu (kama tunaposema amefariki badala ya amekufa), lakini, hususan kabisa ya maiti ni imepatikana, si amepatikana.
mzoga = carcass
Nimekuelewa vizuri sanaMaiti ni i-zi.