Ni ipi nguvu ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar?

Wazanzibari kwenye nchi yao huwa ni wamoja bila kujali vyama. Kwenye maslahi ya Zanzibar huwa wanakuwa kitu kimoja.
 
Lipigwa miti
 
Kunakuwaga na changamoto zipi zinazo chelewesha kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa (SUK) ?
Inakuwaje kila upoisha uchaguzi serikali ya SUK inachukua muda mrefu kuundwa au kuna kudeka na kudekezana?
Hao ACt huwa wanasusia kwa muda ila mwisho wa siku wanakubali. Hiyo ndio sababu kubwa
 
Wazanzibari kwenye nchi yao huwa ni wamoja bila kujali vyama. Kwenye maslahi ya Zanzibar huwa wanakuwa kitu kimoja.
Sababu hawatekani na kuuwana. Huku bara watu wanapenda kumwaga damu za wenzako ndio furaha yao. Mtu anaibuka na kudai wananchi waombe ili Lissu anyongwe. CCM Ina roho mbaya sana, inaamini kwenye mauaji Zaidi.
 
Othman aliyeapishwa Zanzibar kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, ana nguvu gani ya maamuzi akitokea ACT Wazalendo?

Anaweza aka command nini?
Ni upinzani au ni mshirika wa CCM
Au ni stooges tu lipolipo as long as anapata vingora na mihela?
Ni swali la msingi; lakini jibu lake nalo siyo gumu kivile.

Ni fursa tu ya baadhi ya watu kujipatia mwanya wa kunufaika na jasho la walipa kodi.

Labda katika kuchangia maoni ya wengi watakaochangia hapa; nami ngoja nikujibu kwa kuuliza swali kwako na wasomaji wako:
Hivi ni ajenda gani ambayo waliishikia bango hao ACT na kuiingiza serikalini ili ipate kutekelezwa kama mchango wao kwa jamii?
Kama ipo, naomba nifahamishwe.
 
SUK ni ulaghai umefanywa na watawala kupunguza joto la kisiasa Zanzibar lakini ikihakikishwa kuwa CCM haitoki madarakani.
Kila baada ya miaka mitano kuna kiini macho cha uchaguzi ambao matokeo yake yashaamuliwa kabla.
Bila mabadiliko bara wapinzani Zanzibar wataendelea kuburuzwa tu. CCM Zanzibar wanaogopa katiba mpya kuliko wenzao wa Tanganyika.
 
Mkuu Tlaa, Tlaatlaah ,asante sana kwa kuliweka hili vizuri, na haswa hili la kiburi, ujeuri, ubinafsi na majivuno yake, lazima abadilike ili Dr. Mwinyi akiondoka ile 2030 kuja huku, huyu aweze kupewa kule!.

Naikumbuka vizuri post yako hii kumhusu mtu huyu na kiburi chake na jeuri yake,
ni muhimu pia huyu muungwana akaacha ubinafsi na kiburi ambacho ni changamoto kubwa mno pia kwa ustawi wa demokrasia, umoja na amani ya Wazanzibari wachapakazi na itapendeza zaidi πŸ’
Naunga mkono hoja, kiburi si maungwana!, uungwana, ustaarabu, uvumilivu, ustahimilivu na uelewa ni tunu muhimu kwenye kutatua mtanziko wowote wa jambo lolote.

Huyu mwamba OMO, ni kweli ni kiburi!, enzi akiwa AJ wa Zanzibar, nilimshauri Dr Shein Dr. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii
Baada ya Dr Mwinyi kumfanya VP-1 wake, pia nikashauri Ushauri wa Bure kwa Dkt. Hussein Mwinyi: Mfute Kazi Haraka Othman Masoud Kabla Hajaendelea Kueneza Sumu
Baada ya Uchaguzi wa 2025, nikawaandikia makala hii
View attachment 3665813
Nikamshauri Zitto https://www.jamiiforums.com/threads...majina-ya-suk-kususa-hakusaidii-kitu.2413666/

Tunaendelea kusaidia saidia kuwaelimisha watu hawa wabadilike, wasipobadilika, hata 2030 watakula jeuri yao tena na kuishia kula kwa macho na ving'ora!.
P
 
shukrani sana mwalimu P 🀝
 
Othman aliyeapishwa Zanzibar kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, ana nguvu gani ya maamuzi akitokea ACT Wazalendo?

Anaweza aka command nini?
Ni upinzani au ni mshirika wa CCM
Au ni stooges tu lipolipo as long as anapata vingora na mihela?
Tafuta katiba ya Zanzibar utapata jibu sahihi, kinachofanyika kimo kwenye katiba ya Zanziba isipokuwa CCM huingiza ubabe kwenye utekelezaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…