Akizungumza leo Septemba 8, 2026, kwenye Mkutano wa Kitaifa wa Kutafakari hali ya Kisiasa uluiondaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othuman Masoud, amesema Katiba ya sasa ndiyo inahatarisha Muungano wa Tanganyika Zanzibar.
Nukuu ya Maandishi alichokisema Othman Masoud
"ACT swala la mamlaka kamili, nini maana yake?
Mimi nadhani, kama alivyo sema wengine, kwamba mada... kuna mada zinahitaji mimi nadhani mjadala wake pekee yake. Na mimi naamini hili ni moja, kwa sababu msingi wake ni namna tunavyo endesha Muungano wetu.
Tuna mambo ambayo yamo kwenye Katiba, lakini ukitazama, sivyo yanavyo endeshwa kwa mujibu wa Katiba.
Na leo tumefika pahala, mimi niseme hili kwamba kama kuna tishio kubwa la Muungano, ni katiba yenyewe kama tulivyo sasa hivi na kwa namna tulivyo e-frame.
Mimi nasema nieleze kidogo tu. Leo kwa mfano, utakuja kupata bwana Mwabukusi pale, saibu wangu, Rais wa TLS, watu wa nchi hii wamemchagua kwamba yeye ndio Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Na hilo ndio tunalofundishwa katika sheria. Ukitaka kutunga normative framework yoyote, lazima uanze na worst case scenario. Hii sio kwamba ni worst... eh, lakini nasema for purpose ya mjadala. Maana kuna watu hawaamini kwamba Bwana Mwabukusi kuna siku moja anaweza akachaguliwa kuwa... eh, akatoka Rais wa TLS akawa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Lakini akichaguliwa kesho, anaapa kulinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anasema kuanzia Julai mosi, mapato yote yanayokusanywa Zanzibar, kutokana na ushuru wa forodha, kodi ya mapato, na excise duty ambayano yakusanywa na TTRA Zanzibar, haya ni mapato ya Muungano kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Na kwa hivyo, yataingia katika Mfuko Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania badala ya kuingia katika Mfuko Mkuu wa Serikali ya Zanzibar kama utaratibu uliopo sasa.
Jamani, atakuwa amevunja Katiba? Atakuwa amevunja sheria? Sijui ndugu zangu. Lakini mimi ninavyojua, atakuwa amelinda kiapo chake cha kwamba kasimamia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sasa, la pili akasema kwamba bandari zote kuanzia tarehe mosi Julai zitakuwa chini ya TPA (Tanzania Ports Authority). Kwa sababu kwa mujibu wa Katiba wetu, bandari ni jambo la Muungano. Jamani, atakuwa kavunja Katiba? Hajavunja Katiba.
Akisema mapato yote ya uhamiaji ya kuanzia tarehe mosi Julai yaingie katika Mfuko Mkuu wa Serikali ya Muungano.
Akisema Zanzibar mmeunda vyombo vyenu vya kusimamia mafuta na gesi... eh, Serikali ya Muungano ilipitisha sheria mwaka 2015, ambayo inaregulate downstream na upstream kwenye petroleum industry, na Zanzibar na nyinyi sheria ile ikasema kwamba eti na nyinyi mnaruhusiwa na nyinyi kusimamia mambo hayo. Mkaenda kuunda sheria yenu 2016 mkasimamia mambo ya upstream, downstream kama vile yanavyosimamiwa na Serikali ya Muungano kwa upande wa Zanzibar, lakini mafuta na gesi bado ni jambo la Muungano kwa mujibu wa Katiba tuliyonayo ambayo niliapa kuilinda."