Ni ipi njia bora ya kumwachisha mtoto kunyonya maziwa ya mama?


Ehuuuu!!! Nimecheka sana asante kwa ushauri mkuu
 
Ehuuuu!!! Nimecheka sana asante kwa ushauri mkuu

Najiskia ni wajibu wangu kukanusha hayo unayoshabikia....

Kisayansi na evidence toka tafiti mbalimbali ni kwamba maziwa ya mama pekee ndio chakula bora kwa mtoto katika miezi 6 ya mwanzo, kisha analikizwa kwa vyakula vinavyoshauriwa HUKU akiendelea kunyonya maziwa ya mama mpaka miaka miwili au zaidi...angalau miaka miwili. Usidanganyike na 'feelings' za watu zisizo na msingi wowote wa kisayansi na kuathiri afya na ukuaji wa mwanao, hata kumuhatarisha na kifo kutokana na maginjwa mbali mbali sababu mtoto hupata kinga toka kwa mama kupitia maziwa yake. Usimhatarishe mwanao kwa ushauri usio na evidence.
 
Sawa ila nahisi nimechoka kunyonyesha daah

nosimo Umechoka kunyonyesha? Hmmmm kweli tunatofautiana maana mimi kama sio mtoto wangu kufikisha miaka miwili ningeendelea kunyonyesha mpaka akatae mwenyewe. Haupendi bond mnayokuwa nayo sababu ya kumnyonyesha mwanao? Kunyonyesha ni bora pia kwa afya yake!!!

Anyway, if you must anza kwa kupunguza kumnyonyesha. Mimi nilianza kumnyima kunyonya mchana, yani kabisa kabisa, akawa ananyonya usiku tuu. Hapo inabidi ujitahidi kumpa matunda, juice na vyakula vyenye virutubisho vya kutosha. Baada ya muda (alipozoea kwamba biadhara ya nyonyo mchana hamna) nikaanza kumbana na usiku pia. Muda wa kulala nambembeleza alale bila kunyonya, mpaka aje kushtuka na kutaka nyonyo ni usiku wa manane. Akishanyonya hiyo usiku mara moja basi, asubuhi hapati kitu. Alivyozoea hiyo system ndo nikamwambia no more kunyonya. Ilichukua muda ila akazoea.

PS
Ukimwachisha mtoto maziwa jitahidi sana kumlisha vizuri. Yani nyie kama familia kuleni mlavyo ila yeye asikose tunda,mboga mboga, snacks, maziwa kama hasumbui kunywa, vyakula vya protini (nyama,maharage n.k) na vya wanga kwa wingi.
 
Last edited by a moderator:
Sawa ila nahisi nimechoka kunyonyesha daah

Na utakapochoka kumlea..utamuua au utamtoa kwa adoption!? Ulipaswa kujua what you are getting yourself into and if you capable of handling that kabla hujaamua kuzaa. Wanawake wengi huwa wanachukulia watoto kama 'madoli' sijui, wa kushow off, hawajui watoto ni responsibility ya milele...umechoka!? Ebo..
 
...weka nyoya la kuku kene ziwa..ataaacha kunyonya fasta...haahhahahahhahaahah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…