Ni ipi siri ya mafanikio

TIMO MG

Member
Joined
Jan 11, 2014
Posts
12
Reaction score
0
Hello kakaz & Dadaz mko poa? Jamani mi nainshu moja tu, naomba tujuzane ili na mimi nijue, tatizo linalonikabili ni kwamba sijafahamu nini siri ya mafanikio, elimu yangu ni form four,na ni mwaka wa pili nipo nyumbani mara baada ya kushindwa kuendelea na masomo kutokana na kipato duni, nimekuwa nikilima shamba nakupata fedha kiasi, lakini mara nyingi nashindwa kujua nini cha kufanya na hatimaye fedha yote niliyo nayo huniishia. Kuna wakati nafikiria kwamba kufanikiwa katika njia halali ni NDOTO YA MCHANA kwani hata ukiwa ni msomi bado utafanya udhalimu tu, Fani niliyonayo ni kutetengeneza muziki pamoja na kuimba na nimekuwa nikihudumu kama organist kanisani.So ndugu zangu wana JF wenzangu, naombeni mawazo yenu, nifanye je?
 

use your internal talent. pamoja na kulima jaribu pia kuinvest muda wako kwenye muziki.
 
Bado huna dhamira yakweli ktk utaftaji, muda ndio huu usingoje mpaka uzeeke. Huko ulipo jaribu kutembelea sehemu zenye miradi midogomidogo na usisite kuhudhuria semina za kijasirimali. Kumbuka kutumia dhana bora za kilimo na uchague zao zuri la biashara na usiwe mwepesi wa kuuza mazao yako km soko halina tija! Jitanue kila mwaka kadri unavyofanya mambo yako na la mwisho muombe Mungu wako na usikate tamaa ktk ufanyalo cz mafanikio hayaji kwa siku1.
 
Kwa kujazia hapo nikwamba.
Usipende kujitenga peke yako,kaa na watu wenye uono ili uige na upate ushauri wa mbinu za kufanikiwa,maana mafanikio hayana kanuni maalum zaid ya KUJITAMBUA kwanza wewe mwenyewe.

Na Tatizo ulilonalo ni kukata tamaa,na pia nahisi kwamba unataka pesa nyingi kwa pamoja,anza nahicho kidogo,usidharau hata Sh: 200,wapo watu wanatembea kwa mguu sehem ndefu sana kwa kukosa nauli tu,kwahiyo heshim sana pesa,na hiyo ndio falsafa ya wahindi,hata sh:50 hakuachii.

kama umeweza kukiri kwamba kilimo kinakupati pesa kidogo,muhim kiendeleze kilimo chenye tija,achana kabisa na muziki utakupotezea muda,fanya mziki kama sehem yako ya mapumziko na sio ajira,utapotea huko nam uda utakuwa umekwisha potea mwengi.

Muziki utakupoteze muda hasa kwa Level yako na maihsa uliopitia.

Akili yako yote wekeza kwenye Kilimo chenye Tija,weka akiba na pia lima kwa kuangalia soko.
 
fanya kilimo alafu weka akiba punguza starehe au acha kabisa muziki ufanye kama hobby tu.
 
jiwekee malengo lima bidhaa inayolipa na yenye uhakika wa soko iga kwa waliofanikiwa sikushauri sana mambo ya muziki
 
1) Jitambue unataka nini maishani mwako. Kuwa na mali nyingi na umaarufu au mali kiasi na maisha mazuri!
2) Jiwekee malengo yanayo tekelezeka. Kuna malengo ya muda mfupi na muda mrefu. Yatekeleze kwa siku, wiki, mwezi na kwa mwaka!
3) Fanya kazi kwa bidii na ufanisi wa hali ya juu. Acha ubabaishaji kwa kila jambo unalolifanya, itakuharibia jina katika jamii
4) Fanya uchunguzi japo kidogo wa kila jambo unalotarajia kulifanya. Itakufanya kuwa na uhakika wa matendo na kukuepusha na hasara.
5) Weka akiba ya fedha inayolenga kutekeleza malengo makubwa na ya muda mrefu.
6) Hakikisha kila siku unafanya jambo lenye impact katika malengo yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…