TIMO MG
Member
- Jan 11, 2014
- 12
- 0
Hello kakaz & Dadaz mko poa? Jamani mi nainshu moja tu, naomba tujuzane ili na mimi nijue, tatizo linalonikabili ni kwamba sijafahamu nini siri ya mafanikio, elimu yangu ni form four,na ni mwaka wa pili nipo nyumbani mara baada ya kushindwa kuendelea na masomo kutokana na kipato duni, nimekuwa nikilima shamba nakupata fedha kiasi, lakini mara nyingi nashindwa kujua nini cha kufanya na hatimaye fedha yote niliyo nayo huniishia. Kuna wakati nafikiria kwamba kufanikiwa katika njia halali ni NDOTO YA MCHANA kwani hata ukiwa ni msomi bado utafanya udhalimu tu, Fani niliyonayo ni kutetengeneza muziki pamoja na kuimba na nimekuwa nikihudumu kama organist kanisani.So ndugu zangu wana JF wenzangu, naombeni mawazo yenu, nifanye je?