Hahaaa. Ni kweli. anapangilia kiingereza chake vizuri hadi unavutiwa kuendelea kusoma hukumu yake. Amekaa sana pale Commercial Division kabla ya kuwa promoted kwenda mahakama ya rufaa. Kule aliamua kustaafu kwa hiari kabla ya mda wake kufika baada ya kuona junior judge kapewa ujaji mkuu na kuwaacha wakongwe wakitazamana tu. Almanusra majaji wote wa rufaa waachie ngazi, bahati nzuri diplomasia ilifanya kazi yake, majaji wengine wakakubali kubaki, Dr. Bwana akakimbilia mahakama ya kimataifa, jamaa kalegeya kaamua kustaafu kwa hiari. Hatakagi mambo ya mchezomchezo.
Mwingine kwenye mambo ya lugha ni P. A. Rugazia. Huyu jamaa anapamba kiingereza hadi raha. ana vi terminology vyake hivyo ukiiona tu hukumu utajua huyu ni Mwamba Mwenyewe Rugazia, Mzee wa misimamo - haogopi mabosi zake. Jamaa kasota sana mahakama kuu ingawaje alikuwa ni kichwa, hakubahatika kuwa promoted kwenda mahakama ya rufaa. Wengi wanasema ni sababu ya kiburi na majigambo yake. Kastaafu hivi karibuni (mwaka jana kama sikosei).