Ni jambo gani lilikupa nguvu kubwa na hali ya kupambania riziki pale ulipopitia ugumu wa maisha?

Ni jambo gani lilikupa nguvu kubwa na hali ya kupambania riziki pale ulipopitia ugumu wa maisha?

Jchris14

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2019
Posts
801
Reaction score
2,057
Wasalamu wakuu!

Niwape hongera na pole kwa hustling za kila siku za kuhakikisha wewe binafsi na watu wako wa karibu wanafurahia juhudi zako.

Nimeleta andiko hili najua si mara ya kwanza yaweza kuwa lilishaandikwa kwa namna nyingi na wadau humu jukwani.

Hali ya kimaisha inazidi kuwa ngumu siku hadi siku, najua kwa namna moja ama nyingine kila mtu ana mbinu ama story ambayo ilimpa nguvu na hali kubwa ya kupambana hadi alipofikia kujiweka katika nafasi nzuri ya kujihakikishia ameupunguza ugumu wa maisha kwa kiasi kikubwa.

Hali hii ya ugumu wa maisha imewafanya watu wengi waone hata suala la kuoa na kuwa na familia ni anasa.

Sasa enyi ma-malejendi na wakongwe tupeni mbinu ama story zilizowafanya muupunguze huu ugumu. Jambo au story yako inaweza kuwa silaha kubwa ya kumtoa mtu mwingine sehemu moja kwenda nyingine.

Asanteni sana na karibuni 🫶
 
Mpenzi wangu, Kaka mzuri. Huyu mtu amepambana sana kuniweka sawa kiakili, kunikumbusha mimi ni nani na nina uwezo wa kufanya nini. Niliinuka na kutazama mbele kwa imani, hatimaye nikavuka.

Amenifunza sio kila changamoto inahitaji utatuzi wa kifedha, wakati mwingine faraja ndio kitu tunahitaji zaidi tunapopitia magumu.

Mtu anayekupa amani na utulivu wa akili amekupa vyote.
 
Nlianza chuo kikuu nikiwa nmepewa mkopo 100% enzi za mwendazake, kufika mwaka wa 3 presha ya ajira ikaanza kunitesa nawaza nikitoka hapa ntaishije na ajira siku hizi hamna?. Japo nlikuta nshasevu hela kidogo nikiwa mwaka 1&2 lakini mwaka wa 3 nikazidisha ubahili.

Asee Mlo ni mmoja tu kwa siku tena 1000, sikununua nguo mpya hata moja, MB sinunui nikakomaa na VPN no matter what, nikaanza na ujasiriamali kidogo nasevu faida. Nakuja kutoka chuo hela ikatosha kuanzisha biashara japo nilikopa kidogo kujazia.

Thank God inaenda vizuri mwaka wa 4 sasa. Sijutii kujitesa, ningekuwa na confidence ya maisha nisingefanya hayo.
 
Mpenzi wangu, kaka mzuri.
Huyu mtu amepambana sana kuniweka sawa kiakili, kunikumbusha mi ni nani na nina uwezo wa kufanya nini. Niliinuka na kutazama mbele kwa imani, hatimaye nikavuka.

Amenifunza sio kila changamoto inahitaji utatuzi wa kifedha, wakati mwingine faraja ndio kitu tunahitaji zaidi tunapopitia magumu. Mtu anayekupa amani na utulivu wa akili amekupa vyote.
Kongole kwa kaka mzuri
 
Utulivu wa nafsi! Pamoja sana mkuu.
 
tupeni mbinu ama story zilizowafanya muupunguze huu ugumu.
Marekani wana kikosi chao maalumu kinachoitwa Navy SEAL, moja kati ya mazoezi yao ni kuzamishwa chini ya maji kwa dakika kadhaa (Hazizidi tano).Yaani unatakiwa uelee ukiwa chini ya maji na siyo juu ya maji!

Yaani unatakiwa ukae chini ya maji kwa kuelea kwa hizo dakika bila kuibuka juu na bila msaada wa mashine ya kupumulia! Nini utafanya ili umalize hilo zoezi salama utajua mwenyewe!

Wengi hushindwa na miongoni mwa sababu zinazowafanye washindwe ni:

1) Ukijaribu kuja juu utatumia nguvu nyingi na utachoka mapema.

2)Ukijaribu tena oksijeni yako inazidi kupungua!

Walioweza wanasema unatakiwa utulie kisha huo utulivu utakupa njia!

Funzo kwenye maisha:

1) Ukipata tatizo lolote lile, jambo la kwanza ni utulivu. Huu utulivu utakupa njia. Hapa wanamaanisha ni kuukubali ukweli!

2)
Ukipata tatizo kisha ukaamua kulitatua bila utulivu unajitengenezea njia ya kukaribisha matatizo mengine na makubwa zaidi! Hapa wanamaanisha ni kuukataa ukweli!
 
Nlianza chuo kikuu nikiwa nmepewa mkopo 100% enzi za mwendazake, kufika mwaka wa 3 presha ya ajira ikaanza kunitesa nawaza nikitoka hapa ntaishije na ajira skuhizi hamna?. Japo nlikuta nshasevu hela kidogo nikiwa mwaka 1&2 lakn mwaka wa 3 nkazidisha ubahili asee Mlo ni mmoja tu kwa siku tena 1000, skununua nguo mpya hata moja, MB sinunui nikakomaa na VPN no matter what, nkaanza na ujasiriamali kidogo nasevu faida. Nakuja kutoka chuo hela ikatosha kuanzisha biashara japo nlikopa kidogo kujazia. Thank God inaenda vzuri mwaka wa 4 sasa. Sijutii kujitesa, ngekuwa na confidence ya maisha nisingefanya hayo.
Pongezi sana kwako mdau.
 
Marekani wana kikosi chao maalumu kinachoitwa Navy SEAL, moja kati ya mazoezi yao ni kuzamishwa chini ya maji kwa dakika kadhaa (Hazizidi tano).Yaani unatakiwa uelee ukiwa chini ya maji na siyo juu ya maji!

Yaani unatakiwa ukae chini ya maji kwa kwa kuelea kwa hizo dakika bila kuibuka juu na bila msaada wa mashine ya kupumulia! Nini utafanya ili umalize hilo zoezi salama utajua mwenyewe!

Wengi hushindwa na miongoni mwa sababu zinazowafanye washindwe ni:

1) Ukijaribu kuja juu utatumia nguvu nyingi na utachoka mapema.

2)Ukijaribu tena oksijeni yako inazidi kupungua!

Walioweza wanasema unatakiwa utulie kisha huo utulivu utakupa njia!

Funzo kwenye maisha:

1) Ukipata tatizo lolote lile, jambo la kwanza ni utulivu. Huu utulivu utakupa njia.Hapa wanamaanisha ni kuukubali ukweli!

2)
Ukipata tatizo kisha ukaamua kulitatua bila utulivu unajitengenezea njia ya kukaribisha matatizo mengine na makubwa zaidi! Hapa wanamaanisha ni kuukataa ukweli!
Asante sana mkuu kwa ushauri wako! UTULIVU 🤝
 
Wasalamu wakuu!

Niwape hongera na pole kwa hustling za kila siku za kuhakikisha wewe binafsi na watu wako wa karibu wanafurahia juhudi zako.

Nimeleta andiko hili najua si mara ya kwanza yaweza kuwa lilishaandikwa kwa namna nyingi na wadau humu jukwani.

Hali ya kimaisha inazidi kuwa ngumu siku hadi siku, najua kwa namna moja ama nyingine kila mtu ana mbinu ama story ambayo ilimpa nguvu na hali kubwa ya kupambana hadi alipofikia kujiweka katika nafasi nzuri ya kujihakikishia ameupunguza ugumu wa maisha kwa kiasi kikubwa.

Hali hii ya ugumu wa maisha imewafanya watu wengi waone hata suala la kuoa na kuwa na familia ni anasa.

Sasa enyi ma-malejendi na wakongwe tupeni mbinu ama story zilizowafanya muupunguze huu ugumu. Jambo au story yako inaweza kuwa silaha kubwa ya kumtoa mtu mwingine sehemu moja kwenda nyingine.

Asanteni sana na karibuni 🫶
..."jambo gani lilikupa nguvu na ari ya kupambania riziki"...
 
Nikikumbuka bado nina kazi ya Mungu bado sijaifanya kwa asilimia zote, kupitia rizki anayonipa.

Nikikumbuka bado sijafanikiwa kwa ajili ya mama yangu.

Nikikumbuka kuwa nina familia inanitegemea.
Mkuu hakuna kukata tamaa, na mwenyezi Mungu akutie nguvu.
 
Baadhi ya ndugu wa babayngu walitutenga baada ya baba tu kufariki mambo ya mirathi sio mchezo

Kiukweli wamenifanya niwe na hasira na maisha nikiwa mdogo sana
Nikajifunza Kuishi na watu Baki
Nikajifunza uvumilivu
Nikajifunza kupambana nikajifunza kuacha kulia lia binadamu hawana huruma

My mom pamoja na kuwa first lady wakat huo 😀 na Mimi kuwa princess baada ya madadiliko alipita nayo hakuyaonea aibu maisha
Alipambana sana alinifundisha kukubali muda na nyakat kutoka kula tunachokitak had kula kinachopatikana

alinifundisha kusamehe kias nimekuwa konk siwez chukia mtu jamni naweza tukanwa nikacheka tu 😀

Nowdays ni mtu naeweza Kuishi popote ba Kuishi na yoyote
Nina utulivu wa kutosha kwenye haya maisha
Alhamdulillah 🙏
 
Baadhi ya ndugu wa babayngu walitutenga baada ya baba tu kufariki huyu mmoja alidiriki had kufake watoto alijua atapat mirathi
Kiukweli wamenifanya niwe na hasira na maisha nikiwa mdogo sana
Nikajifunza Kuishi na watu Baki
Nikajifunza uvumilivu
Nikajifunza kupambana nikajifunza kuacha kulia lia binadamu hawana huruma

My mom pamoja na kuwa first lady wakat huo 😀 na Mimi kuwa princess baada ya madadiliko alipita nayo hakuyaonea aibu maisha
Alipambana sana alinifundisha kukubali muda na nyakat kutoka kula tunachokitak had kula kinachopatikana
Nowdays ni mtu naeweza Kuishi popote ba Kuishi na yoyote
Nina utulivu wa kutosha kwenye haya maisha
Alhamdulillah 🙏
Mh! Mkuu pole na hongera sana. Hapa ndio ule usemi husema "adui yako hatoki mbali".
 
Back
Top Bottom