Ni jambo gani lilikupa nguvu kubwa na hali ya kupambania riziki pale ulipopitia ugumu wa maisha?

Ni jambo gani lilikupa nguvu kubwa na hali ya kupambania riziki pale ulipopitia ugumu wa maisha?

Nlianza chuo kikuu nikiwa nmepewa mkopo 100% enzi za mwendazake, kufika mwaka wa 3 presha ya ajira ikaanza kunitesa nawaza nikitoka hapa ntaishije na ajira siku hizi hamna?. Japo nlikuta nshasevu hela kidogo nikiwa mwaka 1&2 lakini mwaka wa 3 nikazidisha ubahili.

Asee Mlo ni mmoja tu kwa siku tena 1000, sikununua nguo mpya hata moja, MB sinunui nikakomaa na VPN no matter what, nikaanza na ujasiriamali kidogo nasevu faida. Nakuja kutoka chuo hela ikatosha kuanzisha biashara japo nilikopa kidogo kujazia.

Thank God inaenda vizuri mwaka wa 4 sasa. Sijutii kujitesa, ningekuwa na confidence ya maisha nisingefanya hayo.
Hongeraaa mno
 
Mpenzi wangu, Kaka mzuri. Huyu mtu amepambana sana kuniweka sawa kiakili, kunikumbusha mimi ni nani na nina uwezo wa kufanya nini. Niliinuka na kutazama mbele kwa imani, hatimaye nikavuka.

Amenifunza sio kila changamoto inahitaji utatuzi wa kifedha, wakati mwingine faraja ndio kitu tunahitaji zaidi tunapopitia magumu.

Mtu anayekupa amani na utulivu wa akili amekupa vyote.
Yapendeza kuwa na mtu wakuegemeza bega Pindi maisha yanapokupiga teke
 
Back
Top Bottom