Nakupa pole mshikaj wangu maana hata mimi nakerwa sana na hiyo lugha ya 'ni jambo jema.....'
Lugha hii imeshapata pacha wake. Upo msemo unaotumiwa sana wa '.....ifike wakati......' Kila nikisikia hii lugha nahisi kichefuchefu. Waziri Mkuu wetu ni mtaalamu sana wa hizi lugha na kila akianza kuzungumza kama ni kwenye redio au tv, mara moja nazima au kutafuta kituo kingine.