'Ni jambo jema' inakera.

'Ni jambo jema' inakera.

Zumbe Kimweru

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2014
Posts
340
Reaction score
27
Sio siri wakuu kwa sasa kuona viongozi wakubwa serikalini na hata wasomi wakitoa lugha hii hata kwa vitu visivyo na ulazima utasikia "NI JAMBO JEMA". kwakweli ni lugha ama sentesi inayouzi kuzingatia kuwa hutolewa kipindi ambacho watu huhitaji maelezo ya kiongozi. Kwa mfano unatajwa uraisi ni Jambo jema ukawa wakirudi " Ni jambo jema" Mzee wetu Pinda amekuwa muasisi japo wapo kina dr Bana na vigogo.Yaani mtu hawezi kuzungumza hata maneno matano bila kusema "NI JAMBO JEMA' Duuu ni kweli ni jambo jema!!!! Inaudhi sana kama hunielewi basi NI JAMBO JEMA"
 
Jambo jema hata mimi inanikera sn...hawa wazee ...kero sana...
 
Nakupa pole mshikaj wangu maana hata mimi nakerwa sana na hiyo lugha ya 'ni jambo jema.....'
Lugha hii imeshapata pacha wake. Upo msemo unaotumiwa sana wa '.....ifike wakati......' Kila nikisikia hii lugha nahisi kichefuchefu. Waziri Mkuu wetu ni mtaalamu sana wa hizi lugha na kila akianza kuzungumza kama ni kwenye redio au tv, mara moja nazima au kutafuta kituo kingine.
 
Back
Top Bottom