Ni jambo zuri Serikali inavyohimiza tupande miti ila napendekeza ingehimiza tupande miti ya matunda kama machenza mpaka katika barabara zetu

Ni jambo zuri Serikali inavyohimiza tupande miti ila napendekeza ingehimiza tupande miti ya matunda kama machenza mpaka katika barabara zetu

FrankLutazamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2018
Posts
448
Reaction score
409
Serikali yetu pendwa inaendelea kuotesha maelfu ya mbegu za miti kwa ajili ya kupandwa, pendekezo langu wangekuwa wanapanda miti ya matunda inayodumu na kuchanua kama mipera, machenza, michungwa na kadhalika hata katikati ya majiji katika barabara badala ya miti isiyo zalisha matunda. Ila katika mahali pa kupumzikia ndio ipandwe miti ya kivuli.
 
Mm nataka kupanda miti home. Ushauri wa miti gani mizuri kuweka nyumbani.
 
Ili tugongwe na magari sisi darasa la 7 C tukitoka class.?
 
Mm nataka kupanda miti home. Ushauri wa miti gani mizuri kuweka nyumbani.
Miti ya matunda: michungwa, milimao, mipera na mipapai.

Hiyo utakuwa na uwezo wa kuitunza kwa karibu.

Kwa mfano, michungwa na milimao inahitaji umwagiliaji usiokoma ndiyo ikutolee matunda matamu muda wote, hainaga msimu wa kuzaa, ilimradi ipate maji tu.

Pia michungwa na milimao inatengeneza vivuli vya kutosha kupumzikia.

Ningeshauri mwembe, lakini mti huu unahitaji nafasi kubwa kama ilivyo kwa mkungu.

Sasa kwa viwanja vyetu vya mjini, miti hii ni mizuri lakini ni kitendawili kutokana na eneo.

Kama una kiwanja kikubwa chenye ukubwa wa medium ama low basi waweza panda mwembe ajili ya kivuli na matunda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali yetu pendwa inaendelea kuotesha maelfu ya mbegu za miti kwa ajili ya kupandwa, pendekezo langu wangekuwa wanapanda miti ya matunda inayodumu na kuchanua kama mipera, machenza, michungwa na kadhalika hata katikati ya majiji katika barabara badala ya miti isiyo zalisha matunda. Ila katika mahali pa kupumzikia ndio ipandwe miti ya kivuli.
Kabisa tena jiji kama la Dodoma ningependekeza ipandwe mizabibu kandokando mwa barabara na katikati mwa mtengano wa barabara.
 
Back
Top Bottom