Ni Japan Ama Nairobi? Otamatsuri 2026 Yavuta Maelfu na Kuteka Mtandao

Ni Japan Ama Nairobi? Otamatsuri 2026 Yavuta Maelfu na Kuteka Mtandao

Omu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
469
Reaction score
95
“A Japanese idol concert in Kenya.” Video moja tu yenye maneno hayo imegeuka kuwa gumzo mtandaoni, ikionyesha umati wa Wakenya ukiimba, kuruka na kushangilia kwa nguvu wakati msanii wa Japan akitumbuiza Nairobi.

Video hiyo ilinaswa wakati wa Otamatsuri 2026, tamasha la anime, manga na pop culture lililofanyika Agosti 22 katika Carnivore Grounds, Nairobi. Tukio hilo lilikusanya zaidi ya watu 4,000 kwa siku ya cosplay, gaming, Japanese food, music na live performances.

Miongoni mwa waliopanda jukwaani alikuwa YURAPICO, Japanese solo idol anayejitambulisha kama “the most passionate idol in the world.” Baada ya performance yake, alisema ilikuwa mara yake ya kwanza Afrika na kwamba nguvu na mapokezi ya mashabiki wa Kenya yalimfanya hadi atokwe na machozi.

Lakini hakuwa msanii pekee kutoka Japan. Otamatsuri pia ilileta MIRAISKIRT⁺, ambaye amewahi kutumbuiza Kenya hapo awali, pamoja na Karen wa Colorful Scream, aliyefanya performance yake ya kwanza barani Afrika. Kundi la samurai na ninja Katanaya Ichi pia lilikuwa sehemu ya wageni wa mwaka huu.

Kilichowashangaza wengi mtandaoni si tu kuona Japanese idol akitumbuiza Kenya—bali kuona kwamba Kenya tayari ina community kubwa inayofuatilia anime, manga na Japanese pop culture kwa kiwango hicho.

Otamatsuri, ambayo imekuwa ikiandaliwa Nairobi tangu 2019, sasa inaonyesha jinsi subcultures ambazo zamani zilionekana kuwa niche zinavyojenga communities kubwa nchini.
 

Attachments

  • Jeffrey_J._Hall__________-_A_Japanese_idol_concert_in_Kenya_iZDe3I.mp4
    10.3 MB
Back
Top Bottom