Ni jina gani la "classmate" wako ukilikumbuka linakuvunja mbavu

Ni jina gani la "classmate" wako ukilikumbuka linakuvunja mbavu

Nishato Mbana.....huyu bwana alikua Mzambia.. Ilikuaga ni shangwe hapo assembly mwalimu mkuu akiita jina lake!!
 
BAHARIA WAZIRI jaamaa alikuwa NOMA SANA enzi zetu TOSAMAGANGA HIGH SCHOOL 1984
 
Semeni Shamba...tanga technical hiyo...jina lake lilikuwa likitajwa tukiwa kwenye paredi basi shule nzima tunaitikia ''shaambaaaaaaaaa''
 
Andika Nitoroke...huyu kuna siku alikamatwa na polisi sasa wakati anafunguliwa jalada polisi akamuuliza unaitwa nani..jamaa akajibu :Andika Nitoroke.....hivyo virungu vilivyofata hapo mpaka polisi wanakuja kujua ndo anavyoitwa hivyo...too late..
 
Back
Top Bottom