Ni jukumu la mzazi hasa Baba kumtafutia Kijana wake Connections za Kazi

Ni jukumu la mzazi hasa Baba kumtafutia Kijana wake Connections za Kazi

Ukweli mtupu. Nakumbuka mwaka 2009 nikiwa mwanachuo nilikaa mtaani muda mrefu natafuta sehemu ya kufanya field nilichelewa kama mwezi mmoja. Siku moja katika kumsalimia mzee nikamjulisha mwanao niko town hapa mambo ya field yanazingua.. akaniuliza ngoja nimcheki rafiki yangu fulani nitakurudia. Kama utani mzee ananiambia nitakutumia namba ya rafiki yangu yuko Wizara ya Fedha mpange. Kuja kumpigia yule best wake kumbe ni kigogo mzito mno wizarani. Akaniuliza nataka nianze lini nikamjibu j3 kwa sababu ilikuwa ijumaa hiyo siku. Siku naenda pale wizarani nakumbuka alinishika mkono tukaingia ofisi ya afisa mhusika na pale kwenye bench kulikuwa na RC wa Mbeya enzi hizo anasubiria kuingia. Niliinjoi mno field attachment.

Kikubwa nilichojifunza pia tusiwachukulie poa baba zetu kwa sababu mara nyingi sio waongeaji yaani mikausho mingi. Wana mambo mengi sana.


Iko hivyo.

Wanasiasa ndio watawadanganya watu wenye Akili finyu kuwa Urithi WA mtoto ni Elimu na kuwaambia watoto wa wenzao wajiajiri huko huku wao watoto wao wakiwapa Ajira Nono
 
Hii ni sahihi asilimia kubwa..kilio kikubwa cha ajira Kwa vijana kinatokana na wazazi kupuuzia ukweli huu na kukumbatia ilimu pekee kama ndio urithi.

Vigogo huwezi sikia wakiwaambia watoto wao vitu vya namna hii.
Wao wanachozingatia ni kudhibiti Njia za Pesa
 
kukumbatia ilimu pekee
Ilimu = imani ya Quran tukufu Msikiti Madrasa madufu umbwabwa kaswida Imamu Shekhe Mufti Hustadhi

Elimu = Dunia Mwalimu Mwanafunzi Kiongozi Doktari Nesi Mwanasiasa nk
 
Mtoto anajifunza kwa kukuona wewe sio Maneno matupu.
Ukiweza kumtafutia maisha mwanao kwake ni Somo tosha.

Vinginevyo utaitwa Baba motivation speaker
Again uko very shallow

Sio kuona tu, kusikia, kuthubutu, kushiriki na kuelewa

Uko hovyo blo

Sema ji debe tupu Kwahiyo haliachi kutika

It is unfortunate wenye kamudomo ndio wanaopewa masikio but kaubongo lako finyu kuliko chembe ya haradali
 
Again uko very shallow

Sio kuona tu, kusikia, kuthubutu, kushiriki na kuelewa

Uko hovyo blo

Sema ji debe tupu Kwahiyo haliachi kutika

It is unfortunate wenye kamudomo ndio wanaopewa masikio but kaubongo lako finyu kuliko chembe ya haradali

Ungetoa hoja watu wangekuona wa maana lakini maelezo matupu kwa kweli ni dalili ya mtu mwenye kuwashwa washwa
 
Hamjambo wote!

Majukumu ya Baba yapo bayana. Ushaambiwa Ubaba ni cheo cha juu zaidi Duniani.
Na hakijawa cheo cha juu burebure, hivihivi au kirahisi. Ni kwa sababu ya majukumu makubwa aliyopewa Mwanaume ndiye Baba.

MAJUKUMU YA MSINGI YA MWANAUME AU BABA.

1. Kutafuta Fursa na kujijenga kimaisha.
2. Kutiisha Mazingira yake.

3. Kuunda Connections zenye Tija kwake na kwa kizazi chake.
4. Kuandaa Mifumo ya uzalishaji kwa kizazi chake.
5. Kuandaa Urithi WA watoto wake na kizazi chake.
Sio useme Urithi WA mtoto ni Elimu.
Elimu haijawahi kuwa Urithi mahali popote pale.
Na haupo kwenye Sheria za mirathi.

6. Kuwatafutia watoto Kazi za kufanya na connections za uhakika.

Huyo ndiye Baba na mwanaume.

Majukumu hayo ndio humfanya mwanaume yoyote Makini kutokuwa na Muda WA kufikiri mambo ya kijingajinga au kupoteza Muda kwa mambo yasiyo na Tija.

Baba au mwanaume anayejielewa huwezi msikia akiwambia watoto wake wakatafute Kazi za kufanya.
Ila yeye mwenyewe kama Baba anakuwa ameshaandaa mfumo wa vijana kuwa na Kazi au Kupata Kazi.
Labda mtoto mwenyewe aamue kufanya Kazi zingine Nje ya mfumo wa Baba yake.

Ndio maana familia zote kubwa za Watawala, wafalme, wafanyabiashara Wakubwa, matajiri na watu wote wenye kujua Kanuni hiyo mara zote wazazi hasa Baba huhangaika Kufa kupona kuwaweka watoto wao katika nafasi nzuri za kiuchumi.

Kumpa mtoto Elimu haimsaidii chochote kama hukumpa connections na mfumo wa Kazi.

Wanasiasa wote Duniani hujua Jambo hili tangu Duniani kuumbwa.
Wafanyabiashara na matajiri wote huwezi sikia wakiambiwa watoto wao wakatafute Kazi au wawaache watoto wao wajitafutie malisho kama mayatima wasio na Baba.

Baba husema, mwanangu David umeshakua Mkubwa sasa, chukua Ng'ombe hawa watano, eneo la malisho lipo pale.
Mwanangu Kipeto, kuna shamba heka tano lile la Kule Turiani. Tangu mdogo umekuwa na Mkono wa Kulima. Nenda kalime Mwanangu.

Mwanangu Kibadeni, umesoma Udaktari, utaenda katika hospital ya Plus Tune. Fulani atakupokea. Sasa uende ukanitie aibu huko.

Dunia ilianza na connections na itaisha kwa connections.
Hapa Kati wanadamu walitaka kujidanganya kwa kujaribu kujifunza mambo yasiyo ya Asili.

Hii itupe changamoto kama vijana wa Leo tujue yakuwa Sisi kama Wanaume na Wababa wachanga tunaowajibu wa kupambana Sana. Sana tena Sana kwaajili ya Kesho yetu na kizazi chetu.

Usije ukapotoshwa.
Mzazi ndiye mwenye jukumu la kumuwekea mtoto wake mifumo ya kuishi.na sio vinginevyo.

Mzazi wako akishindwa unaasilimia 80% ya kushindwa katika Maisha.
Wewe ukishindwa maisha kuna asilimia 80 ya watoto wako nao kushindwa.

Sio serikali Wala mtu yeyote mwenye jukumu la kukufanikisha.
Mwenye jukumu Hilo alikuwa Baba yako, na kama ameshindwa Basi jukumu Hilo limebaki juu yako MWENYEWE.

Mama unajukumu la kuhakikisha Baba anasaidia watoto kufika Kule anakotaka.

Wanawake bahati nzuri wanaijua hii natural.
Ndio maana ukishaoa hata kama ndio mpo mwaka wa Kwanza na bado vijana utakuta Mkeo anakushinikiza tujenge mapema kwaajili ya watoto wetu.
Tuanzishe miradi kwaajili ya watoto wetu

Ni jukumu letu kama wanaume au Wababa kutengeneza channel kwa watoto wetu. Huo ndio Ubaba wenyewe.

Taikon Master
Kwa sasa Dar es
Kila mtu afe kivyake.
 
Kuna watu flani jamii ya Kihindi na Waarabu tulipiga nao O-Level.
Katika haraki za ujenzi nikakutana nao kweny Hardware pale Moro😀🙂🙂wahuni wale ni madoni mbaya...waliishia O-Level wakaenddlea na Biashara za familia...nashukuru nilipata discount maana tulikuwa marafiki sana.

Shida tayari kuna gap😀😀😀😀😀
 
Back
Top Bottom