Ni kada wa CCM nisiyetetea kiongozi, naitetea CCM

Ni kada wa CCM nisiyetetea kiongozi, naitetea CCM

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2020
Posts
1,809
Reaction score
1,692
Wanajf, Salaam!

Kwa miaka zaidi ya 40 ya umri wangu nimekuwa mwanaccm kindandaki - siku zote pale CCM ilipoaibishwa na baadhi ya viongozi nilisimama imara kushauri, kukosoa na kutoa maoni. Mfano:

= Wakati wa fukuto la kundi la akina Kinana kutukanwa na baadhi ya viongozi wa CCM, nilikataa utamaduni wa kunakngana kwa madhala yake kwa CCM yangekuwa makubwa;

= Wakati wa uhakiki vyeti feki na mishahara hewa nilikosoa juu ya wanasiasa kutoguswa huku wakiishi kwa fedha za Umma;

= Wakati watu wakipotezwa hovyo nilishauri umuhimu wa maridhiano ya mezani kuliko kuokatili uhai usioweza kuuumba; ikizingatiwa kwamba waliotoweshwa hawakuwa na madhara ya kiusalama kwa taifa;

= Ni wakati wa zuio la mikutano ya kisiasa nilishauri CCM tuukabili upinzani majukwaani badala ya kuukwepa majukwaani;

KATIKA KIPINDI HIKI CHA RAIS SAMIA SULUHU NASHAURI

(i). Serikali kuwa makini na matumizi ya fedha na mali za Umma (nikiona kwa wakati mmoja midege inapaa kutoka Dom - Dar ikiwa na Rais, nyingine wakati huo huo ikapaa kutoka Tan - Malawi / Zambia ikiwa na Rais mstaafu; nyingine wakati huo huo ikapaa kutoka Tan - Burundi ikiwa na WM) hapa napata wasiwasi kidogo juu ya matumizi ya mali na fedha za Umma. Kama upo uwezekano review ifanyike;

(ii). Uwiano wa maisha ya watanzania wa chini dhidi ya viongozi wa watanzania - hapa lipo gap kubwa sana. Wakati wananchi waliowapa dhamana ya uongozi wakiishi maisha ya ukabwela ninyi viongozi mnaishi maisha ya kujipenda nafsi. Mfano, mwananchi hana maji, wewe una mshahara mkubwa na maji unalipiwa; mwananchi hana umeme lkn kiongozi mwenye mshahara mkubwa analipiwa umeme; mwananchi hana simu lkn wewe kiongozi mwenye mshahara mkubwa unalipwa fedha za kugharamia simu; mwananchi analima kwa mikono lkn kiongozi mwaka kwa mwaka huoni sababu ya kugawa trekta kwa vikundi vya wakulima nchini;

(iii). Wewe ni kiongozi unayetumia fedha zitokanazo na kodi ya mtanzania kwa kugawa jezi na mipira kwa kundi la bodaboda badala ya kuwaanzishia SACCO'S ili wakuze mitaji hatimaye waimarishe sekta zingine;

(iv). Wewe ni zao la CCM unayepokea mshahara mkubwa na marupurupu kibao lkn hata fedha za maendeleo ya Jimbo unazilamba, fedha za self-help scheme unazilamba, fedha za own source unazilamba - basi hapo unaichimbia CCM kaburi - unaichonganisha CCM kwa wananchi!

Tuipende Tanzania
Tuwapende viongozi watakao tupenda

Mungu bariki Tanzania
Msakila M Kabende (Economist)
 
Kutokula kitimoto wakati machuzi wake unakunywa bakuli zima
 
CCM kama taasisi yenye watu wenye majina na nguvu haiwezi kubadilika na haitakaa iache asili; mathalani, Makamba katibu, katumia pesa alizozipata kwa jina la chama kumuweka Makamba junior, huyu naye atatumia pesa alizokwisha kwapua kumuweka mwanae anayempika na mchezo utakuwa ukijirudia rudia hivyo kwa wote.

Ilikuwa ni sahihi kuwa na mtu mmoja mwenye nguvu, atakayetawanya mizizi yote kisha atengeneze mifumo, kazi isiyowezekanika kwa miaka 10 tu ya uenyekiti.

Kwenye bwawa la maji taka, hawezi kuibuka msafi!
 
1E5AF209-9E63-4F38-A6D3-AC3131C9D267.jpeg
 
Hoja zako zina mashiko.

Tatizo siyo CCM kwani ni chama cha siasa chenye wanachama ambao wengi wao jasho lao wanafaidi viongozi. Hata vyama vingine vya siasa hali ni hiyo hiyo.

Tatizo ni viongozi wa kisiasa kwa kuwa siasa imegeuzwa kuwa sekta isiyo rasmi ya kujitajirisha. Mifano uliyotoa ni ushahidi wa hoja yangu. Yumkini hata Maprofesa wa fani za kitaaluma (uhandisi, sayansi, afya, fedha, nk) wanaacha kazi ya kujenga jamii kielimu wanakimbilia kwenye siasa.
 
Back
Top Bottom