Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Hivi karibuni mimi pamoja na watu kadhaa wa karibu tumepitia tatizo la kiafya la kummwa na tumbo, kuharaha na wengine kutapika. Huu unaoneka sio ugonjwa wa kawaida ni kama kuna mlipuko wa homa ya tumbo.
Kinachoumiza na kutisha zaidi ni ukimya mkubwa kutoka Wizara ya Afya na mamlaka za serikali za mitaa, ambao hadi sasa hawajatoa tamko lolote la kuwatahadharisha raia wala kutuma wataalamu mitaani kuchunguza chanzo cha janga hili.
Ufafanuzi wa Wizara ~ Dkt. Erastus Sylvanus: Wizara ya Afya haijapata ripoti ya mlipuko wa magonjwa ya tumbo
Mlipuko wa namna hii, ambapo watu wengi wa eneo moja wanapata dalili zilezile kwa wakati mmoja, ni ishara ya wazi kuwa kuna hatari kubwa. Hii inamaanisha kuna chanzo kinachosababisha labda ni maji tunayokunywa, vyakula vya mtaani, au kuna virusi vinavyosambaa kwa kasi.
Hivyo basi, tunaziomba mamlaka kuamka na kuvunja ukimya huu kwa kutoa taarifa rasmi kwa umma kwani ni wajibu wa viongozi kusimamia afya za raia wao, na hatua madhubuti lazima zichukuliwe sasa hivi kuokoa maisha ya watu kabla hali haijawa mbaya zaidi.