Ni kama tunahamasishwa kutakiana mabaya kila wakati

Ni kama tunahamasishwa kutakiana mabaya kila wakati

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,151
Reaction score
4,277
KUNA HAJA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI NA WAHUBIRI KUACHA MASUALA YA KUTAKIANA MABAYA.
Huwa nafuatilia kwa karibu sana nyimbo nyingi za Injili hususani za miaka ya karibuni pamoja na mahubiri ya kizazi cha zama zetu za sasa. Nimeweza kubaini kuwa kuna Injili ya aina ya ajabu sana inayosukumwa kwa njia ya mahubiri na njia ya nyimbo.

Siwezi kutoa jibu la moja kwa moja kuwa ni nyimbo zote au mahubiri yote ndivyo yalivyo la hasha! ila kinachoweza kuonekana hapa ni kuwa kwa kiasi kikubwa kumbo la kuombeana mabaya ni kama limeshika kasi kubwa zaidi. Mahubiri yakusisimua hisia za kusukuma ubaya kwa adui yamekuwa mengi mno. Watafuti mnaweza kuutumia uwanja huu kuliona hili.

Wimbo unaimbwa mwanzo mwisho haumtukuzi Mungu ila unalaani wabaya tu kama kwamba ndiyo jambo la msingi mno kuliko wokovu. Inasikitisha sana leo mpaka shuhuda zinasusimua kwa jujikita zaidi kwenye kulaani wengine. Rejea wapigweee.......

Biblia ninayoiamini Mimi inanielekeza kuwa kisasi siyo kazi yangu ila ni kazi ya Mungu. Yete ndiye mlipaji wa haki. Sasa sisi tunaimba na kujifunza kulipa kisasi kwa kulaani tunautolea msingi wetu wapi?.Tunafurahia tunaodhani ni adui zetu wakifesheheshwa tutafanikiwa, lakini tunafahamu kujiuliza hivi kuanguka kwa tunaowaona wabaya ndiyo mafanikio yetu au mwisho wa ubaya?.

Je hatma yetu ipo mikononi mwa anguko la wabaya?. Naona kama tunainua hisia za ubinafsi na chuki kuliko upendo na umoja. Tunapaswa kufahamu hakuna kilicho na faida Duniani, hata siku ya ubaya ni siku ya kusudi. Unayemuona mbaya kwako anaweza akawa anakusaidia kuliko yule unayemwamini na kumuona mwema.

Tafakari juu ya mfano huu, moto unaweza kuonekana mzuri au mbaya kutokana na matumizi yake au mtazamo wa mtu juu yake. Swali la kujiuliza ubaya upo wapi?. Wakati mwingine moto tunaoutazama kwa mtazamo hasi ndiyo unaotusaidia kusafiri katika vyombo vya moto n.k.
Ubaya unawezakuwa uzuri unaokusaidia ila unaweza kuonekana hausaidii au inasaidia kutokana na mtazamo.

Sisi sote ni nguvu ileile, adhabu ya karma inatembea na kila mtu, ni kwa nini tuisukume nguvu ya asili na usuli wa matendo ya mtu kwa kunuwia vibaya kwa sala, nyimbo na maombi?
 
Back
Top Bottom