Zamani Kulikuwa na AC ngumu mfano SANYO from Japan, LG from Korea, DAIKIN from Japan, CHIGO from China, Kipindi zinakuja bongo hizo AC nilizotaja zilikuwa ni roho ya Paka kabisa, hiyo CHIGO Kipindi zinaanza kuingia bongo zilikuwa balaa yaani Hadi Leo hii zipo zinazopiga kazi, CHIGO za mwanzo zilikuwa n ngumu Sana hazifi Kila kitu kigumu, mchina salute Kwa toleo la mwanzo la chigo, SANYO nae ndio kabisa usiseme...
Kuhusu ishu za kudumu muda mrefu inategemea vitu vingi Sana kuliko materials za AC yenyewe japo ni kweli kuna AC ziko vizuri mfano Zipo Daikin ambazo ni Inverter but ni ngumu Sana, Condenser lake n gumu haliozi wala kupinda haraka, bati zake pia n ngumu Sana lakini nazo zinakufa pia. AC nyingine kama Midea, LG, Samsung sio mbaya, kumbuka AC unaweza Kuta ni kampuni moja lakini model ni tofauti na uimara pia ni tofauti. Kumbuka Kila AC unayoiona ww ina kasehemu kake Ka udhaifu.
AC zinahitaji maintenance kila mara ili ziweze kudumu zaidi, lazima ujue size gani ya AC inatosha Kwa chumba chako na hapo ndio watu wanapofeli, wanaambiwa Tu chukua hiyo kafunge haina shida.
AC zote Inverter changamoto Yake ni kufa Kadi yaani Ile motherboard, zile non inverter ni very simple kurudi kupiga kazi maana haina mambo mengi but inverter kidogo Tu Inakugua gharama kubwa za ukarabati na mafundi bongo ni wababaishaji.
NB: Kila AC unayoiona ww ina kasehemu kake Ka udhaifu, zingatia Hili ninalosema.