Ni katika harakati za kuhuisha, kuchanga upya kama sio kubadilisha kabisa mfumo

Ni katika harakati za kuhuisha, kuchanga upya kama sio kubadilisha kabisa mfumo

Smartkahn

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2020
Posts
594
Reaction score
1,061
Tulikua watu makini kama wa 4-5 ama 6 sikumbuki vizuri... (waandamizi wa jambo flani, sijui ni jambo gani ila ni kama jambo la maana sana)

Tulikua tunakatiza mitaa fulani usiku huko kijijini, tukiwa katika njia ya vumbi inayotosha kupita gari, gafra ukaona kikosi/kikundi cha watu Sita walionekana kuwa sio watu wazuri.

Tulivyolingundua hilo tukaamua kujificha pembeni ya ile njia pale mtaani tulipokua palikua na godown lililokosa gate tukaingia mle ndani ulikua na giza nene tukajibanza ukutani kwa kujilaza katika magunia yaliyokua tupu.

Baada ya muda wale watu kikosi wakafika na wakaingia ndani wakawa wanatutafuta ni kama waliagizwa kutuwinda walingia ndani kabisa mbele kule ya go down wakatuacha nyuma.

Nikaona ngoja niinuke nipambane nao nikawasha tochi nikawamulika na mwanga kumbe hawakuwa watu wa kawaida nikitaka kuinuka nashindwa nikitaka kuongea pia nashindwa nikagundua kuwa kile kikosi kilikua na nguvu za giza😎

Baadae Nikajikuta pekeyangu wale wezangu sikuwaona nikabaki na mmoja wa wale wanakikosi tunapambana ni kama wenzao wlikimbia/wakatawanyika hivyo tukagawana wale watu wakikosi waliwafuata wale wezangu huko walikoenda.

Nilipokua napambana na yule bwana nilikua nimemzidi uwezo (nilimmudu) lakini sikua na silaha au zana sahihi ya kumpigia nilikua nimeshika fimbo ya mzizi wa mti nilikua nampigia na nilikua napiga sehemu ya upande wa kichwa kushoto usawa wa sikio ule lakini kila nikipiga yule bwana hata hashituki... Nikakimbia akanipoteza.

Nilikimbia nikafika mahali pana kibanda kimejengwa kwa miti kikiwa wazi hakijaezekwa kina uwazi uwazi ukiwa ndani mtu anakuona kwa zaidi ya asilimia 98% wakati nikiwa napumzika pale kuna ufahamu ukanijia kua wenzangu wameuwawa(nilijua tu)

Baada ya muda kidogo nikaona wale watu wa kile kikosi baadhi yao walikua kama wa 2-3 hivi walikua wanakuja Nilipokua wakati huo kushakua mchana, nikashangaa. Kumbe pale kibandani ni maeneo yao wanapokutaninaga Kiufupi nilikua kwenye kambi yao, sikuona kilichotokea pale kibandani palipokua pembezoni mwa kile kijiji palipokua kaskazini katika dira.

Sikuona kilichoendelea pale kibandani baada ya wale jamaa kunikuta ila nilijikuta niko mwishoni magharibi kaskazini mwa kijiji nikiwa nakimbia huku nikitafuta sehemu zuli/kichaka cha kujificha huku wale jamaa wakinitafuta nawaona wanavyokuja ila wao hawanioni nimewapoteza.

Basi kule polini mwishoni mwa kijiji kulikua na vichaka migomba na matuta makubwa ni kama tuta lilikua limeshavunwa hivyo kwa juu lilikua flat na limeota magugu mengi ya kijani nikajilaza chali kwenye lile tuta kumbe nguo zangu zote chini hadi juu zilikua za kijani hivyo nikajificha vyema kabisa nikawa ngumu kuonekana nikaongezea na majani mapana ya migomba nikajifunika kwa hali ile nilijua tu kua hawataniona nao waliishia kule kule zinakoishia nyumba wakipita njia ya pembezoni mwa kijiji, ikaishia hivyo.

Nilijua tu wamenishindwa pasipo kua na uhakika nini kilitokea baada ya pale, kama nilivyojua kuwa wezangu wameuliwa pasipo kushuhudia wala kuambiwa...
 
Inawezekana kuna mchawi mmoja kabakia
 
Back
Top Bottom