Ni kauli gani uliwahi kuambiwa na baba, mama au mlezi wako ambayo baadae kabisa ndio ulikuja kuielewa?

Ni kauli gani uliwahi kuambiwa na baba, mama au mlezi wako ambayo baadae kabisa ndio ulikuja kuielewa?

Jobless_Billionaire

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2022
Posts
3,106
Reaction score
8,101
Kwema wakuu?

Binafsi nilikulia kwenye familia ambayo wazazi wanazingatia sana kuhusu watoto wao, nikimaanisha ni watu wenye kufuatilia Kwa ukaribu sana mienendo yetu, sio watu waliotuachaniza kufanya mambo Kwa kujiamulia.

Kipindi nasoma nilikuwa na rafiki zangu ambao wazazi wao walikuwa tofauti kidogo na wa kwangu, yaani ni aina za familia ambazo mtu unaweza kutoka hata ukalale huko huko hakuna mtu atakuuliza. Kiufupi walikuwa huru sana.

Katika urafiki wetu Kuna muda nilikuwa nashindwa kuenjoy sababu nashindwa kufanya baadhi ya mambo Kwa kuhofia muda au jambo husika huenda likazalisha maswali mengi Kwa wazazi wangu ilhali Kwa wenzangu sio issue hata kidogo, hakuna wa kuwafuatilia.

Familia ilikuwa na uwezo wa wastani TU hakuna kitu tuliomba tukakosa.

Siku moja tukiwa shule wale jamaa zangu walikuja na kusema wamepata kazi kiwanda Fulani wanaingia usiku na kutoka asubuhi kisha wanaunganisha kuja shule, mshahara 70000 Kwa mwezi, na Wana siku ya pili tangu waanze. Kwa wakati ule na umri ilikuwa ni pesa nzuri TU, nikawa naona jamaa zangu wanaenda kutoboa kimaisha tukiwa bado tunasoma. Kwa wakati huo sikuweza hata kuwaza kuhusu ugumu wa kazi pamoja na kupata muda wa mapumziko sababu kiuhalisia ni ngumu kuhandle mambo hayo within 24 hrs pasipo mapumziko ya kutosha.

Kichwa kilipata moto sana, Kuona rafiki zangu wana-make na shule wanakuja. Kwakuwa nyumbani siwezi kujiondokea tu ikabidi nijaribu kulifikisha Kwa mzee nikitegemea ataruhusu kwakuwa ni wazo chanya kabisa. Nililifikisha kwake lakini ikawa kinyume na matarajio. Mzee alinigombeza sana na kunielekeza mambo mengi sana, nilikumbana na maswali magumu ambayo majibu sikuwa nayo ila kubwa aliniambia "Jifunze kufanya mambo Kwa wakati, MAISHA YAPO TU SIO YA KUKIMBILIA"

Kiukweli moyoni mwangu sikuridhika, nikaona mzee kanionea. Nikawa najutia kuwa kwenye familia kama Ile ya kukaa wanatubana. Nikahisi mzee hataki kabisa nifanikiwe, ila ndio sikuwa na namna ikawa nimepigwa marufuku.
Jamaa wale hata wiki mbili hazikuishaga wakaacha kule tukabaki kusoma TU.

Sasa Kuna kipindi hayo yote yaliisha, mambo ya elimu, utu uzima Sasa nikiwa najisimamia mwenyewe niliwahi kupigwa na maisha mtaani, kila nlichogusa ilikuwa hola. Nikaamua kwenda kiwanda Fulani, kazi ni ngumu halafu msimamizi katuweka watatu TU ili apunguze cost halafu mashine haizimwi, aisee... Niliishia nusu siku nikatema Bungo hata hela sikuwahi kuiomba.

Alhamdulillah Mungu alibariki, nikavuka kote huko, maisha yamekuwa poa, nimepiga kazi Home Tanzania hadi nilipopata Connection ya kazi Jamhuri ya Czech kwenye moja ya makampuni makubwa ya ujenzi ambapo ndipo nilipo na Watanzania wengine wawili miezi takribani mitatu

Kweli maisha hayakimbiliwi.

One Love...
 
niliambiwa huyo girlfriend niliyenaye siyo wa kwangu na hawezi kuwa mke ,Mama akaniambia soma kwa bidii mke wako Bado hajazaliwa ,ni Kweli aisee hiyo ilikuwa 1997 ,mke wangu niliyemuoa amezaliwa 2000 ,na yule girlfriend wangu ambaye alikuwa ananimaliza akili kwa sasa ni mwenyekiti wa UWT wilaya,na aliwahi kumfundisha my wife secondary,halafu tukisimama na huyo ex wangu naonekana kama Mtu na mama yake mdogo...
 
Sikubahatika kulelewa na baba aliondoka kwenye uso wa dunia nikiwa na 9 mouth so malezi mengi ya uanaume niliyapata kwa babu mzaa mama,kipindi cha sherehe za mwisho wa mwaka alikuwa anachinja kondoo au mbuzi tunajumuika familia nzima kula kufurahi na kujuliana hali.

Alikuwa anapenda kutukusanya wajukuu wa kiume chini ya mikahawa na kusema maneno haya “yeyote siku akijiona amekua,arudi nyumbani“ sisi kwa uchanga wa mawazo tukawa tunaulizana mbona tupo nae hapa hapa kijijini tutarudi kutoka wapi?niliondoka kijijini nikiwa aged 11 niliporudi mwisho wa mwaka kwenye sherehe zile zile akaniita safari hii peke yangu akaniambia tena maneno yale mwaka uliofuata akaniita tena akasema vile vile,ikabidi nimuulize mjomba babu anachomaanisha kwanza akacheka sana akaniambia anamaanisha ukijiona umefikia kuoa usioe nje ya hapa,wazee wanaona mbali sana Mungu aendelee kumtunza Babu huko uliko.
 
Nakumbuka mzee wangu alinambia, unapokuwa bado upo katika harakati za kujitafuta kimaisha hakikisha unazungukwa na marafiki wenye kiu ya utafutaji, itakuwa ni rahisi kufikia malengo na sio kuzungukwa na marafiki ambao wanapenda ushindani sababu watakufanya uspend more money ili uishi maigizo na utapoteza focus yako, na endapo utafanikisha malengo yako, ishi kwa akili na kiumbe kinaitwa mwanamke sababu kuendekeza wanawake na ngono ni chanzo cha umasikini
 
Back
Top Bottom