Pre GE2025 Ni kauli ya Kishamba mno aliyotoa Chalamila, kuwa tarehe 24, majeshi yetu yote yatakuwa yanafanya usafi jijini!

Pre GE2025 Ni kauli ya Kishamba mno aliyotoa Chalamila, kuwa tarehe 24, majeshi yetu yote yatakuwa yanafanya usafi jijini!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwani mkiandamana na majeshi yakifanya usafi, shida ipo wapi nyie CHADEMA?

Mbona Chalamila hajawalalamikia CHADEMA kutangaza maandamano ila CHADEMA mnamlalamikia Chalamila kufanyia usafi Mkoa wake kwa msaada wa jeshi?

Pale Soko la Mabibo, Chalamila aliwahi kuleta wanajeshi wakafanya usafi huku biashara zikiendelea bila bugudha wala mikwaruzano.

Kwa hiyo CHADEMA ninawasihi sana nyie andamaneni tu msiogope, ila mkifanya fujo ninadhani zoezi la usafi litasitishwa kwa muda.
 
Angalia watu wanaoteuliwa alafu utaijua akili ya mteuzi kiufupi hii nchi alipokufa jiwe bora angekufa na msindikizaji wake tunapelkwa pelekwa tu leo uache kuhamasisha hao wanaoandamana wafanye usafi unawaleta polisi na wanajeshi jamaa hana akili.

Jambo dogo tu wangesema fanyeni maandamano ya amani na mfanye usafi maeneo mnapopita hata kuokota taka tu ni usafi alafu hao polisi wasimamie swala la ulinzi mbona angekua kaupiga mwingi tu ila kwakua ni mteulewa mtu fulani na mwafulani naye akili kisoda basi jamaa anaamini kamfurahisha mwafulani

Big brain. Umetoa hoja kubwa Sana.
 
Jeshi letu ni madhubuti sana na linawedi wa hali yajuu sana kwenye medani ya vita, sema tu tuna baadhi ya wanasiasa w ajabu ajabu. Wala tusiliaumu Jeshi hata kidogo Jeshi letu linaheshims kubwa sana Duniani.

Ni aibu sana kwa kauli ya Chalamila. Amelitumia jeshi Kama scapegoat.
 
Kama dhamira ni usafi basi Waaze leo na sio kusubiri mpaka TAREHE 28
Mbona CHADEMA walisubiri siku Samia kaenda Hanang na wao ndiyo wakafanya ziara the same day?

Hii ni michezo yao hao wanasiasa wanajuana wasitupotezee muda.
 
Kwani mkiandamana na majeshi yakifanya usafi, shida ipo wapi nyie CHADEMA?

Mbona Chalamila hajawalalamikia CHADEMA kutangaza maandamano ila CHADEMA mnamlalamikia Chalamila kufanyia usafi Mkoa wake kwa msaada wa jeshi?

Pale Soko la Mabibo, Chalamila aliwahi kuleta wanajeshi wakafanya usafi huku biashara zikiendelea bila bugudha wala mikwaruzano.

Kwa hiyo CHADEMA ninawasihi sana nyie andamaneni tu msiogope, ila mkifanya fujo ninadhani zoezi la usafi litasitishwa kwa muda.

Chalamila kaingia kwenye mtego wa CHADEMA mapema Sana. Huwezi jua huo mtego wa CHADEMA una maana gani, yeye kaingia kichwa.
 
Mbona CHADEMA walisubiri siku Samia kaenda Hanang na wao ndiyo wakafanya ziara the same day?

Hii ni michezo yao hao wanasiasa wanajuana wasitupotezee muda.

Kwa hivyo unakubali JWTZ wanatumika kisiasa na CCM.
 
Kati ya Chalamila ambaye katoa kauli kuwa tarehe 24 ni siku ya usafi Dar es salaam na Magufuli ambaye alizuia Maandano na mikutano ya siasa kwa miaka yote ya utawala wake huku yeye akifanya kila siku nani mwovu zaidi?
Mimi naona lawama na laana zote atupiwe Magufuli muasisi wa ushenzi katika nchi iliyostaarabika
Magu keshaenda zake. Tusonge mbele. Chala hafai hata kuwa mkuu wa kata.
 
Kati ya Chalamila ambaye katoa kauli kuwa tarehe 24 ni siku ya usafi Dar es salaam na Magufuli ambaye alizuia Maandano na mikutano ya siasa kwa miaka yote ya utawala wake huku yeye akifanya kila siku nani mwovu zaidi?
Mimi naona lawama na laana zote atupiwe Magufuli muasisi wa ushenzi katika nchi iliyostaarabika
Duh!
 
Kwani chalamila kazuia msiandamane
Wanaolalama humu sio waandamanaji au tuseme wabongo waoga kuandamana kama kawaida yao ndio maana kuambiwa tu jeshi litafanya usafi siku hiyo basi teyari washaogopa.

Hakuna waandamanaji hapo.
 
Aliyekwambia USAFI unaingiliana na MAANDAMANO YA CHADEMA ni nani? Wao si waendelee na maandamano yao wakati usafi unafanyika Shida iko wap? ACHA UOGA
MIMI NIPO NA MAJESHI YETU KUFANYA USAFI
 
  • Kicheko
Reactions: Tui
Hayo ni yako dhamira ni kufanya usafi ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu.
Mnafanya usafi kwa matukio. Ndio maana magonjwa ya kipindupindu hayaishi. Issue ndogo TU ya usafi wa mazingira imeishinda serikali na wananchi kufanya kama utaratibu wa kila siku hadi kipindu×2 kije ndio tunajua kufanya usafi. KWA KWELI MWAFRIKA NA UCHAFU NI KAMA CHAI NA SUKARI
 
Nimestuka sana nilipoisikia kauli aliyotoa mkuu wetu wa mkoa wa Dar tena kanisani, kuwa tarehe 24, "anawaagiza" askari Polisi 5,000 na askari wa JWTZ 8,000 wajitokeze mitaani Dar, ili wafanye usafi!

Kustuka kwangu ni kuona Mkuu wa Mkoa, asivyoelewa majukumu ya Hawa walinxi wetu, Kwa kuwa Jeshi la Polisi nchini, wajibu wake namba moja ni kuwalinda Rais na Mali zao na JWTZ wajibu wao namna moja ni kulinda mipaka ya nchi yetu.

Nimuulize Mkuu wa Mkoa, Chalamila, hivi Kwa kuwataka hao Polisi wetu na askari wa JWTZ wafanye usafi wa Jiji, siyo kukiuka Katiba ya nchi?

Huyu aliyetoa kauli hii ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa Dar na pia ameitoa kauli hiyo akiwa kanisani na ametoa kauli hiyo, baada ya kumsikia Mwenyekiti wa Chama kikuu Cha siasa nchini Cha Chadema, kutoa kauli kuwa hiyo tarehe 24 watafanya maandamano ya amani, ambayo ni haki yao kikatiba kwa kuitaka serikali kuiondoa bungeni miswada 3 ya Sheria, Kwa kuwa hiyo miswada ni kiini macho!

Huyo Chalamila ndiye anayejaribu kuivunja Katiba ya nchi waziwazi Kwa kutaka kuleta taharuki nchini, Kwa kuwa siku hiyo aliyoyaagiza majeshi ya ulinzi nchini yaingie mitaani na kufanya usafi, ndiyo siku hiyohiyo ambayo Mwenyekiti wa Chadema ametangaza kuwa wanategemea kufanya maandamano ya amani.

Najua kuwa Chalamila, ametoa kauli hiyo ili kuwatisha wafuasi wa Chadema, wanaotarajia kuandamana siku hiyo, waingie hofu ya kuandamana.

Yeye Chalamila anajua fika kuwa taarifa aliyotoa Mwenyekiti wa Chadema, ni halali kabisa, Kwa kuwa ndani ya Katiba yetu ya nchi, inaruhusu kufanyika maandamano ya amani.

Hivi tukisema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, ndiye anayetaka kuleta uvunjifu wa amani ya nchi hii, nitakawa nakosea kweli?

Nimalizie Kwa kusema kuwa, kama amani ya nchi hii itapotea, basi Mkuu wa Mkoa wa Dar, awajibike Kwa kuitumbukiza nchi hii kwenye umwagaji wa damu.

Tunamwomba Mungu aendelee kuilinda nchi hii, kutokana na hao viongozi wa Chama tawala na serikali yao, kutokana na hila zao za wakati wote za kutaka kuendelea kuitawala nchi hii bila kutaka kuondoka madarakani Kwa amani
Mkuu nimeelewa nini unamaanisha .

Nikijulishe mkuu kuwa ukimuona nyani kariakoo basi ujue kuna aliye mleta Kariakoo.

Hiyo kauli haikutoka kwa bahati mbaya au karopoka.

Huyo ni waya wa spika tu
 
Hayo ni yako dhamira ni kufanya usafi ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu.
Ccm mmekuwa ni waoga sana kwa cdm na mnakuwa wa kwanza kukimbilia kwa wanajeshi.

Ila lazima mjue kuwa kuna siku hata hao wanajeshi watakataa huo usanii wenu
 
Back
Top Bottom