LA7
JF-Expert Member
- Aug 26, 2019
- 655
- 2,369
nimekaa nikawaza kwa jinsi nilivo na wakati mgumu sasahivi huku nikifikiria kuwa shida yangu kwa sasa inaweza tatuliwa tu kwa laki mbili,
lakini kuna mtu ameweka mamilioni benk au wamechimbia chini au mara nasikia jinsi watu wanavokula na kuishi kwa kupata kila kitu kwa kodi zetu huku sisi tukifanya kazi ngumu zaidi yao, hata tukisema tukaombe mikopo hatupewi kisa tu hatuko kwenye mfumo wa serikali, mbona kodi tuna lipa wote? mara ukipita ofisi za uma unaona jinsi mali za umma zimeharibika wala haziwezikarabatiwa tena kwani zimepitwa na wakati zimerundikana tu huko stoo japo zaweza wafaa watu wengine,
ukitaka kuamini dunia haina huruma waulise wale omba omba pale mjini watu wangapi huwapita hawana hata muda nao, najua haiwezekani kumsaidia kila mtu ila kila mtu anaweza kumsaidia mtu,
kuna wakati namshukuru mungu kwa hatua hii kwani kila siku nikiamka najua kabisa siku yangu naenda kushinda kwenye kaofisi changu, kwani asubuhi huwa nakutana na vijana kama mm lakini wao wanaishi na ndoto zilizokufa wanasubiria wazazi wadondoke wagawane urithi.
dunia tunapita. mtu akikuletea shida au kukuelezea shida yake jitahidi umsaidie bila kufukiria pia usipende kutoa msaada utegemee faida hapo hujatoa msaada, mm bnafsi huwa nasaidia kadri ya uwezo wangu.
ofisi yangu ni ndogo lakini kuna watu wanafunzi wawili nawafundisha kadri ya uwezo wangu japo mm sijawa master sana, hawanilipi zaidi ya mm kuwapa kidogo tunachopata kwa ajili ya kula mchana na sabuni kwani momja ni anafamilia kabisa,
hakuna shida mbaya kama ambayo inakuhusu ww na mtu mwingine iwe kwa bahati mbaya au makusudi,
mfano: kugongesha gari ya mtu au kupoteza pesa ya mtu, kiujumla kumsababishia mtu hasara ambayo itakulazimu kufidia kwa namna yoyote hata ikibidi uende jela.
ntarudi kuandika humu ijumaa maana kwa namna yoyote ile ufumbuzi utakuwa umepatikana,
naomba nikuachie swali kwako, ni hasara gani ulisababishiwa na mtu mwingine ukaamua tu kumsamehe?
kwangu mm zipo nyingi tu ila huwa ikitokea naangalia kama huyo mtu anaweza kuchangia kama hawezi huwa namsamehe tu toka nijitambue sitaki kumlipisha mtu labda tu achangie au yeye mwenyewe aseme kwamba atachangia pia mm nitaangalia kama huo uwezo anao.
samahani kwa kuwachanganyia mada bado nimevurugwa huu mwaka kama ni kitabu basi kitakuwa na kurasa tu za kutosha sio mchezo.