Ni kiasi gani kikubwa cha fedha ulishawai mkopa mtu? Je alirudisha

stritglow

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2018
Posts
622
Reaction score
1,750
Haijalishi ni ndugu, rafiki, jirani nk lazima kila mtu alishawaiombwa hela na mmoja kati ya hao watu.Hilo ni jambo la kawaida. Kuna mwingine anaweza kukuomba umkopeshe kiasi kidogo, ambacho unaweza hata hujifikirii mara mbili kumpa, ila kuna mwingine anaweza kukujia na request ya kukuomba hela ndefu ambayo inaweza ikawa hata juu ya uwezo wako au ambayo usiwe comfortable kumpa.

So kama mada inavyosema ni kiasi gani kikubwa cha fedha mtu alikuomba umkope? je ulimpa? na kama ulimpa, je alirudisha hiyo hela?
 
Aisee kiasi kikubwa kilikuwa laki tatu ila mpaka leo tunazungushana na kukimbizana tu kama couple ya vipepeo mpaka nimejuta.
 
Kuna Rafiki yangu mpk leo sitaki hata kumuona kisa laki2 tu, nilimkopa laki2 akaahidi mwisho wa mwezi, ikapita miezi4 nikimkumbusha anasema jamaa yangu si ufanye kama umetoa sadaka tu, nikamwambia kwahiyo huna nia ya kunirudishia!? Nikasema haina noma Jamaa yangu na mawasiliano nikavunja kabisa
 
Ukitaka kuvunja undugu au urafiki kopesha hao watu. Nishakopesha kiasi ambacho hata nasikiaga aibu kusema kuwa mtu amenirusha kiasi hicho.
 
naweza kukopa kwa nia ya kuirudisha nikipata, lkn mara nyingi naona usumbufu kurudisha deni bila kufatwa.
 
Mm nilimkopa member wa jf nilishamlipa lakini ilikuwa milioni 2
Cc: Mwifwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…