Ni kichapo gani ulichokipokea kutoka kwa wazazi enzi za utoto wako ambacho hautokisahau?

Ni kichapo gani ulichokipokea kutoka kwa wazazi enzi za utoto wako ambacho hautokisahau?

Me nilikuwa mtoto wa kike ila kampani zangu wavulana....sababu ndo waliokuwepo mtaani..basi nikajifunza utundu wote wa kiume mpk kuyega ndege...kupanda juu ya mti wakiwa wamelala jioni tunawakamata then tunawafuga..tulishakula shorwe sana tu...

Sasa siku moja nilipewa adhabu shule kwa utundu..ilibidi Morning niamke nitengeneze wali na mabaki ya chakula nikayasonga kama ugali then nikamwaga sehemu ambayo napiga mswaki..then nikamuamsha mother kumwambia najisikia vby nimetapika..wacha apaniki na kunipeleka hosp badala ya yeye kwenda kazini....enzi zile ukipimwa malaria lazima utaambiwa unayo na wengi walikuwa wanapima clinically..basi bwana shule nikaombewa ruhusa huku wenzangu wakitumikia adhabu ya kuchimba shimo wiki nzima.

Siku ya zote nilizokuwa home..mama akienda kazini tu na me natoka kwenda kicheza nikiona anakaribia kurudi na mie najirudisha najilaza kama naumwa na dawa sikuwa nameza

So ikafika siku tukaenda kuangua mapera mto fulani upo milima ya uluguru...pembezoni mwa huo mto kuna mpera una mapera ..so kama kawaida nikapanda..kufika juu si kuna nyuki...nikaanza kuumwa na nyuki na kuanza kulia huku nawafukuza kwa mikono..ni Mungu tu ile mpera ulikuwa na matawi yaliolala na niliyeenda kucheza nae alikuwa somehow mkubwa kwangu so alipanda fasta kuja kunidaka then tukaseleleka kushuka chini...kumbuka chini kulikuwa na Bonge na jiwe yale ya miamba na bonge kubwa la mto..ningeanguka pale ingekuwa nishakuwa historia

Basi akanipeleka kwao akanibembeleza mama yake akanipa huduma ya kwanza..nikalala kabisa..mama aliporudi home tulipanga tumwambie kuwa tulikuwa tunapita basi nyuki alituuma...basi aliporudi nikamwambia akiumia sana na akanirudisha hospitali kutibiwa tena...

Ile siri ilikuja kugundulika baadae kumbe kuna mtu alikuwa shamba la mlimani alituona na alikuwa anakimbia kuja kuniokoa...alipogundua tumeshuka akaendelea na ishu zake..so one day alikutana na mother akamwambia kila kitu...hakuna siku niliyochezea viboko kama hivyo na sijawahi kuchapwa tena..na sitokaa nisahau viboko vya siku ile..mpk nilisema ukweli kuwa nilikuwa na tabia ya kutengeneza matapishi ili nisiende shule....ujinga mzigo
 
Duu kisa changu siwezi kukisema kilikua cha beki tatu wakati ndio sijui nabalehe .....aloooo! yule mzee alipiga bana !

Nilikua naskia kwamba ukimshika mwanamke maziwa analegea ,nilitoka speed kama ngiri nikaning'inia kwenye maziwa ya beki tatu nikijua namlegeza kumbe namuumiza ,alinisemea bana maana ilibidi apelekwe hospital hicho kipigo sitokaa nikisahau
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji31]
 
Tulilelewa na dingi kwa kuwa mama alienda zake abroad kusoma tangu mimi na mdogo wangu tukiwa wadogo kabisa, kwahiyo dingi alilazimika kuwa mpole tu nafikiri alikuwa anatuonea huruma.

Sasa mimi nikajua dingi ni mshkaji tu hamaindi chochote. Kila siku alikuwa anarudi saa mbili usiku ndio mimi naenda kuoga nae. Siku hiyo namsubiri nipo sebuleni nakula mziki wa Alfa Blondi, dingi akatia timu kama kawa, akaenda moja kwa moja kwenye redio akaroa tape yangu akaweka mabolingo yake

Mimi kuona hivyo nikajifanya Tundu Lisu nikamuambia "hivi baba wewe ni mjinga sanaee, kwanini umezima nyimbo yangu?" dingi aligeuka na sura fulani hivi nikajua tu hapa nimekinukisha. Wadada wa kazi walikuwa jikoni wakaona tumekatiza hapo jikoni kama Tom na Jerry ikabidi wamtulize mshua kwamba usiku ule isingekuwa poa maana nyumba ilikuwa na fensi ila haina geti

Usiku ule nililala na wale wadada maana dingi alikuwa na nia ya kunifanya kitu mbaya

Kulipokucha nikasahau msala wa jana usiku nikamfuata kama kawa anapojiandaa nakuwa naye, kumbe yeye bado ana fundo aisee, nilikula kipondo kitakatifu na hapo watu hawanisaidii wala nini. Hadi leo wadogo zangu ambao walikuwa hawajazaliwa kipindi hicho wananitania na stori hiyo ys kumuita baba mjinga
Alikuwa baba rafiki sana sasa na ww ukajikuta ni kama age mate wako [emoji23] [emoji23] [emoji23] akakuonyesha yy ni baba
 
Back
Top Bottom