Ni kigezo gani kinatumika kuwaita waliopigana vita kuu ya dunia mashujaa?

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Hatuwezi kuwaita waliotumika chini ya mkoloni mashujaa bila kuwaita wakoloni wenyewe mashujaa.

Mnatuchanganya?

Yapo mambo mengi mmeyaficha katika historia, hamuwaambii wananchi kuwa wapo ndugu zetu walihusika katika biashara ya watumwa kwa kuwakata ndugu zao na kuwauza kwa wageni.

Wakati mababu zetu wanateswa na wakoloni, wapo ndugu zetu waliokuwa wamekaa upande wa wakoloni wakiwatesa ndugu zetu.

Hatuwezi leo hii kulaani ukoloni huku tukiwatukuza waliokuwa wakifanya kazi chini ya wakoloni.

Ninachojua mimi, Tanganyika wala Zanzibari hazikupigana katika vita kuu ya dunia bali wapo watu waliochukuliwa kwenda kupigania wakoloni katika vita hivyo.

Hivyo kama taifa hatuna shujaa yeyote aliyepigana vita kuu ya dunia kama hatukushiriki katika vita hivyo.
 
Ni hoja yenye ukweli kabisa, hatukashifu wazee wetu ila ni ukweli ulio wazi, walienda kupigania maslahi ya wakoloni na sio maslahi ya nchi yao, hivyo hawaingii ktk orodha ya kina Mkwawa na Kịnjeketile
 
Hatuwezi kuwaita waliotumika chini ya mkoloni mashujaa bila kuwaita wakoloni wenyewe mashujaa.

Mnatuchanganya?

Yapo mambo mengi mmeyaficha katika historia, hamuwaambii wananchi kuwa wapo ndugu zetu walihusika katika biashara ya watumwa kwa kuwakata ndugu zao na kuwauza kwa wageni.

Wakati mababu zetu wanateswa na wakoloni, wapo ndugu zetu waliokuwa wamekaa upande wa wakoloni wakiwatesa ndugu zetu.

Hatuwezi leo hii kulaani ukoloni huku tukiwatukuza waliokuwa wakifanya kazi chini ya wakoloni.

Ninachojua mimi, Tanganyika wala Zanzibari hazikupigana katika vita kuu ya dunia bali wapo watu waliochukuliwa kwenda kupigania wakoloni katika vita hivyo.

Hivyo kama taifa hatuna shujaa yeyote aliyepigana vita kuu ya dunia kama hatukushiriki katika vita hivyo.
WW2 ilikuwa ni imperialists War. Wakoloni wao kwa wao ndio walipigana, kwenye vita kuu ya pili ya Dunia, Tanganyika tulikuwa chini ya Mwingereza. Kwa hiyo wavulana/Vijana walichukuliwa kwenda kupigana vita kwa colonial masters. Wakati wa African nationalism hawa Vijana/wavulana walijulikana kama The returning Ex-soldiers/Veterans wa ww1na WW2. Hata babu yangu alikuwa ni Ex soldier wa WW2 Ilifarika mwaka Juzi 2020 akiwa na umri wa miaka 98. Kwa hiyo hawa the returning ex soldiers wa ww1 na WW2 hawakuwa mashujaa kwa Tanganyika ispokuwa walikuwa mashujaa/heroes wa mjerumani na Mwingereza. Mashujaa wa Tanganyika walikuwa akina MKWAWA OF HEHE na wengine ambao waliupinga ukoloni usiku na mchana.
 
Walishakufa hizi kelele hazina lolote muhimu kuwajali walio hai kwa sasa, maslai mabovuu kwa police walio hai ila wakifa eti mashujaa. Ila fresh tuendelee tu mashujaa wetu na mnara mpya wajengewe
 
C C M. mbona nayoo kama mkoloni tu, C C M isivyokuwa na adabu na ilivyozoea udhulumaji wa haki za wananchi wa TZ siku tukianza kutumia ARTIFICIAL INTELLIGENCE katika kufanya kazi mbalimbali CCM wataifanyia udhulumaji teknolojia hiyo
 
ego kwa kweli unawakosea heshima wazee wote waliopigana vita ya pili ya dunia:

1. Hawakwenda kwa hiari yao, ni mfumo uliokuwepo ndiyo uliowatuma na hata wewe ungekwenda

2. Walipokwenda na kuona nini kinafanyika ndiyo wakatanabahi na kujua kwamba kumbe wazungu nao wanaweza kupigwa na kushindwa kabisa. Na hapo ndipo walipoamka na kuanza kupigania uhuru wa nchi zao.

Na hii haikutokea kwa Tanganyika tu bali kwa nchi nyingi ambazo zilikuwa makoloni ya wazungu, kwa kweli waliwaamsha waafrika kwa kuwapeleka kupigana vita ile.

Uhuru unaoringia leo ni kwa sababu ya wale wazee ambao sasa unawaona kama walikuwa vibaraka wa wazungu.
 
Tambua mzungu alikua akifa,kipindi kile cha ukoloni,maiti yake ilikua inafichwa ili waafrika wasijue kua wazungu hufa pia,hawa maaskari walioenda kupigana,katika kushiriki kwao,walikuja kujua kumbe hawa wazungu wanakufaga,walivyorudi waliwapa moyo wale waliokua wanapigania Uhuru,kwa kuwaambia kua,hawa tunawaweza,tukishindwa kwa njia ya diplomasia,tunaweza kuwapiga kwa bunduki au zana nyingine zozote,na tukawashinda.Although hii ni minor point,naona kweli wanaotakiwa kuwa mashujaa,ni wa Kagera tu.
 
ego kwa kweli unawakosea heshima wazee wote waliopigana vita ya pili ya dunia:

1. Hawakwenda kwa hiari yao, ni mfumo uliokuwepo ndiyo uliowatuma na hata wewe ungekwenda

2. Walipokwenda na kuona nini kinafanyika ndiyo wakatanabahi na kujua kwamba kumbe wazungu nao wanaweza kupigwa na kushindwa kabisa. Na hapo ndipo walipoamka na kuanza kupigania uhuru wa nchi zao.

Na hii haikutokea kwa Tanganyika tu bali kwa nchi nyingi ambazo zilikuwa makoloni ya wazungu, kwa kweli waliwaamsha waafrika kwa kuwapeleka kupigana vita ile.

Uhuru unaoringia leo ni kwa sababu ya wale wazee ambao sasa unawaona kama walikuwa vibaraka wa wazungu.

Hoja siyo kwenda kupigana kwa hiari au la, hoja ni kusema mashujaa wetu waliopigana vitana vitana kuu ya pili ya dunia wakati sisi hatukupigana vita hiyo.

kama hawa waliokwenda kupigana vita kuu ya dunia ndiyo walikuwa chachu ya kudai uhuru, basi tutawatambua kama mashujaa kwa kudai uhuru na siyo kupigana vita kuu ya dunia.

Tunapiga kelele, elimu yetu mbovu, sijui tulikosea kuruhusu wazungu kuandika historia yetu lakini on ground tunaonekana sisi wenyewe kutokujua ni kitu gani sahihi cha kufanya.

Mpaka leo hii bado tunawafundisha watoto wetu sijui nani alikuwa gavana wa kwanza wa kiingereza, sijui alitawala mwaka gani mpaka mwaka gani? mtoto wa primari.

Tufike mahala watoto wetu waelewe tu kuwa maisha yetu kabla ya kuja wakoloni yalikuwaje, mifumo ya kiutawala, hali za maisha ya kiuchumi na kijamii katika jamii zetu.

baadae walikuja wakoloni, je walibadilisha vipi maisha yetu kutoka mifumo iliyokuwepo, je mifumo ya maisha iliyokuwepo kabla ya ukoloni ilikuwa na mapungufu gani yaliyopelekea sisi kutawaliwa?

Baadae tuliendesha harakati za ukombozi, je ni kwanini tuliingia kipindi hiki? yawezekana ilitokana na kujitambua, yawezekana ilitokana na kuchoka dhuluma, yawezekana ilitokana na baadhi yetu kwenda katika nchi za hao wanaotutawala na kujifunza mambo mengi kama vile wapiganaji wa vita kuu ya dunia na wasomi waliokwenda kusoma.

Baadae tulianza kujitawala, je mifumo ya maisha ilikuwaje katika kujitawala.

Katika mchakato huo wote tunachokitaka ni watoto wetu waelewe wao wana mchango gani katika kulinda utu wao, kulinda uhuru wao, kuboresha mifumo ya maisha ya kiutawala, kiuchumi na kijamii. watoto waelewe Tunaposema "dunia imekuwa kama kijiji", kwa maana huko nyuma tunasema wasomi na wapiganaji wa vita ya dunia walivyochangia kufungua upeo wa watu baada ya kufika kwa wenzetu, leo hii kupitia utandawazi kila mwananchi anaweza kutambua kinachoendelea dunia nzima bila kuhitaji kuhamasishwa na mtu aliyefika huko, je watoto wetu wanatumiaje fursa ya utandawazi kuboresha hali za maisha yetu huku walikinda uhuru wetu na utu wetu?

Tunayo nafasi ya kubadiri fikra juu ya historia yetu.
 
Sasa kwani nani amewakataza Tanzania kusomesha historia inayoeleweka?

Hata ikiwa tulitawaliwa na akina nani na nani lazima vizazi vyetu viyatambue yale yaliyotokea bila ya kufichwa. Wenzetu wanafundisha historia proper iwe nzuri iwe mbaya lakini sisi tunachagua nini tunataka kufundisha na kipi cha kuwacha. Hiyo si sawa hata kidogo.

Kuna baadhi ya historia ya nchi mimi nilikuja kuelezwa na Mjerumani mmoja mpaka niliona aibu maana hatukuwahi kufundishwa mashuleni na enzi zetu hakukuwa na youtube wala mitandao kwa hivyo unalosomeshwa shuleni ndiyo hilo.

Bado nina imani kuwa wazee waliopigana vita vya pili vya dunia ni mashujaa hata kwa mchango wao wa kumtokomeza Hitler ambaye hatujui angetufikisha wapi yule jamaa.
 
Back
Top Bottom