Ni kipi chanzo na tiba ya misuli ya jicho kutikisika?

Nasema

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2010
Posts
556
Reaction score
344

Wadau wa JF Doctor naomba mnisaidie.

Kwa kipindi cha takribani wiki mbili sasa jicho langu la kushoto limekuwa linacheza sana sehemu ya juu (inayoshikilia kope) na kusababisha jicho zima kucheza hadi wakati mwingine nalazimika kulifumba kwa muda. Hali hii imekuwa inatokea kwa vipindi tofauti kwa wastani wa kama kila baada ya dakika 45 hivi. Nini maana yake na nifanyeje ili nitatue tatizo hili?

Natanguliza shukrani.

WADAU WENGINE WENYE KUHITAJI UELEWA WA TATIZO HILI
Heri ya mwaka mpya,

Wadau ninapatwa sana na hali ya jicho kucheza na si jicho hasa bali ni hii part ya juu ambayo inabeba kope yaan imekuwa ni kero na sijui husababishwa na nini na pia ningependa kujua dawa yake.

Naomba kuwasilisha.
Asante

MICHANGO YA WADAU

 
Ngoja wataalamu wapitie huku watatueleza, nasubiria majibu kwa hamu hata mimi ninatatizo kama lako.
 
Nina tatizo kama hilo pia. Jicho hilohilo na muda takribani ni huo huo, niliuliza watu wakaniambia kiimani kwamba nitaona jambo litakalonisababisha nilie.ulipotokea msiba wa kanumba likatulia kwa siku mbili likaanza tena mpaka leo sasa sijui nini kitatokea au ni imabi tu.
 
Mi mwenyewe nina tatizo kama hilo zaidi ya miaka kumi sasa linanitokea hadi nimekuwa mshirikina yaani najua likicheza namna fulani basi jambo baya litatokea, namna nyingine ntapata kitu kizuri na mara nyingi huwa kweli in another side tatizo hili kitaalamu huitwa tics yaana kunakuwa na involutary movement of muscles hasa facial muscles na kuna dawa zake ila sijabother kuzikariri maana sioni shida yoyote.
 
"KWA KIASI (95%) KIKUBWA ISHARA ZA JICHO LAKO HUTOA KAMA IFUATAVYO"
Mara nyingi jicho huashiria kuona kitu cha furaha(mfano mshiko/pesa) kwako kama linacheza juu kushoto
Kama chini mara nyingi huashiria kulia/kutoa machozi ya uchungu/kuna huzuni inakukakiribia
Kucheza kulia juu mara nyingi huashiria kuona mwili mfu/mwili wa aliyekufa
Kucheza kulia chini mara nyingi huwa ni kicheko/furaha ya kucheka hadi machozi kutoka

" KAMA LINEMANISHA VIZURI OMBA MUNGU AKUPE MWONGOZO NA KAMA LINAEMANISHA VIBAYA OMBA MUNGU AKUEPUSHE HUZUNI/SHARI INAYOKUJA MBELE YAKO"
 

Hayo maoni kama yako hata mimi nishayasikia sana ingawa kwa kweli sijayatilia sana maanani lakini nakubaliana na wewe nafikiri hii haitofautiani sana na nyayo kuwasha au mguu wa kushoto au kulia wengine watakuambia una safari au una wageni wanakuja na viganja kuwasha au mkono wa kushoto watakwambia kuwa utapokea chochote kizuri na ikiwa mkono wa kulia basi wewe ndio utatoa.
 
Heri ya mwaka mpya,

Wadau ninapatwa sana na hali ya jicho kucheza na si jicho hasa bali ni hii part ya juu ambayo inabeba kope yaan imekuwa ni kero na sijui husababishwa na nini na pia ningependa kujua dawa yake.

Naomba kuwasilisha.
Asante
 
Pole sana mi mwenyewe huwa inanitokea mara kwa mara lakini badae linaacha!
 
Hapo kuna mgeni au zawadi inanukia
 
Usivae mavazi mekundu. Ukilala elekea kusini.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Itaisha baada ya muda mfupi. Ni inbalance tu ya cations mwilini, itajirekebisha yenyewe. Usiiunganishe na imani yoyote. Pole, huwa inakera kweli!

Ni kweli hili wengi huhusisha na imani za ajabu ni mucheza kwa misuli ya jicho... occular muscles spasm
 
Dawa yake ndogo sana,likianza kucheza tu we zima muziki litaacha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…