Ni kipi hutokisahau ulipokuwa ukweni?

Ni kipi hutokisahau ulipokuwa ukweni?

Nilienda ukweni huko kwa wasukuma,sijui walinilisha manini wale watu nikavimbiwa asee...
 
I'll never forget such kind of moment in my life. Ile wamepika matoke wakayachanganya na maharage, plus matumbo ya ng'ombe, karanga za kusiginwa plus karanga za kutafunwa, humo humo mfuru, kha! Ile siku nilitembea kama naruka majoka vile kuelekea toy kujiharishia, tena mbele ya mama mkwe na madada wa muke wangu

Choo kilikuwa na katundu ka kuchungulia nje ukiwa umechutama, nikitamani waondoke nianze yangu, lakini ndo kwanza wako kwenye kijikeka mbele ya choo. Ile kuchutama tu, walisikia Buuuuuuuum Bhaaaaa Pah! Kila mmoja wao alikuwa mbele ya tukio alikimbia kama mchwa kichaa, mama mkwe alikimbia akiwa ameweka mikono kichwani huku akiuficha mbichwa, wakina dada walikimbia huku wameziba midomo yao ili kuizuia cheko, mke wangu pekee ndiye aliyebaki eneo la tukio akivumilia hali ile ya milipuko ya mabomu ya Mbagala kwa huruma nyingi mno

Nilivyotoka tu chooni, niliwasha bolt nikaondoka zangu, mke wangu alinifuata akiwa na virago vyetu. Huo ndo ulikuwa mwisho wa kutembelea ukweni

Mola awabariki sana wake zetu

Ila mtoto wa mama mkwe atakuja kuua jitu humu ndani
Ila we jamaa🤣🤣🤣🤣
 
Mie nilipatwa na msiba wa Mzee w wife nkafika huko Tunduru ndani ndani Sasa pombe za kimjini hazipo karibu iliyopo ni gongo ya korosho si ili kutoa soni nkapiga bwana we ikawa kesi ,kumbe ile pombe ni noma saaana aisee ikawa vurugu mechi msiba wote naonekana mm tu badla ya kutoa soni ikawa nimefanya soo hatari ,ukweni Kuna mambo
 
😂😂😂 Halafu ukute muda huo unasutwa, umevaa zako shati la mistari halafu umechomekea, plus smartphone kiganjani huku ukiwa siriazi kama wasoma habari ITV, we acha tu mkuu, mambo mengine yanaumiza sana

Same applied to this one 👉 - YouTube
 

Attachments

  • Screenshot_20240815-073220.jpg
    Screenshot_20240815-073220.jpg
    178.4 KB · Views: 2
Mimi Kwa wakwe naenda saa 12 jion.naondoka saa 2:00 usiku. Sipendi ujinga,, ikija kutokea nimelala Kwa mkwe ujue Kuna MSIBA wa mtu wa ndani sana
Itakuwa umeoa karibu na kwenu,utoke dar alafu useme nakaa sa 12 jioni hadi sa mbili usiku
 
Back
Top Bottom