Ni kipi kilifanya Juma Nature kuwa spesho kuliko wasanii wengine wa kipindi chake?

1. yuko real sana cz hta kwenye nyimbo zake huongelea vitu vya kitaa ambavyo tunaishi
2. mtaalamu wa kujiongeza (wewe mpe chorus ndio utamjua vizuri ) ana sauti zaidi ya tatu
3. anafanya aina tatu za mziki; bongo flave, hip hop na rap cartoon
4. hana maringo kuanzia kwa fans hadi kwa wasanii wenzake
5. ana NYOTA kali sana
 
No offence:
Mimi binafsi naonekanaga mpinzani
sikuwahi kuona ukali wake hata naonaga kawaida tu...Nature yuko overrated

Haujakosea. Muziki wa Juma Nature ulikuwa ni muziki wa kisela zaidi. Muziki wa kiume. Warembo wengi ule ulikuwa sio muziki wenu. Nyie enzi hizo mlikuwa mnamshobokea MB Dog, Lady Jay Dee na Mr. Paul.
 
Haujakosea. Muziki wa Juma Nature ulikuwa ni muziki wa kisela zaidi. Muziki wa kiume. Warembo wengi ule ulikuwa sio muziki wenu. Nyie enzi hizo mlikuwa mnamshobokea MB Dog, Lady Jay Dee na Mr. Paul.
Mkuu Tofautisha usela na mziki wa kiume
mbona mimi huyu nilikua shabiki wa Wana hiphop wengi sana wakina Langa /wateule nk nao walikua wanaonekana wagumu kipindi hicho, tatizo ni kutokua shabiki wa kitu anachoimba msanii.
Nature kwangu atabaki kuwa msanii wa kawaida tu kama wengine Akina Chege /Dully nk kwa sababu sikuwahi kuona kitu extra kwa upande wangu kwakweli.
 
Namba 5 Hapa ndio sababu yenyewe
jamaa ana nyota tu
 
Hii nayo roho mbaya
 
Haujakosea. Muziki wa Juma Nature ulikuwa ni muziki wa kisela zaidi. Muziki wa kiume. Warembo wengi ule ulikuwa sio muziki wenu. Nyie enzi hizo mlikuwa mnamshobokea MB Dog, Lady Jay Dee na Mr. Paul.
Na Top In Dar
 
Ile pumzi na spidi ya ku rap.kwenye hili.game..hakuna msanii anayeweza kufanya vile kwa sasa..hawa kina joh makini anaimba maneno.mawili anahema ..necha alikua next level.. bana hebu sikiliza ile chorus ya niko gado.na zay b? Alivuta pumzi halafu akaachia then skiliza kilichofuata... stive b necha venture ni mafundi wa kukeshaaa halafu halafu anapiga kamluzi... mtu.mmoja mambo milioni.moja achana kbs na yule mndengereko... kingine necha alikuwa anaupenda tu muziki na alikuwa hafanyi kibishoo mpaka watu wanashangaa star mkubwa yupo simple namna ile.. necha akiwa star kbs alikuwa anatembea kwa miguu toka temeke mpaka kkoo..jamaa alikuwa wa kipekee yule.. na alikuwa yupo tayari kuimba na yoyote bila zengwe.. kifupi kwa tabia kama zile lazima uwe tu mtu wa watu
 
1. Anajua kuimba
2. Hardworker
3. Kiki
4. Wanawake
5. Good Performer (jukwaani)
6. Anajua watu wanataka nini kwa wakati gani
7. Collabos na wasanii wakubwa
Umetisha aisee!! nakubaliana na uliyoyaorodhesha hapo. Na mie cha kuongezea tu ni kwamba, jamaa pia yuko na "connections" sahihi za wadau wa muziki TZ.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Taja wasanii wako watano (5) wa enzi hizo ambao uliokuwa unawakubali wewe.
 
Nakumbuka one day Mshua alinikuta nasikiliza "Hili Game" akaniuliza wimbo unahusu nini, nimtajie mistari miwili mitatu nikabaki 😳😳😳
 
Rap katuni style... iliyojikita zaidi kureflect maisha halisi ya watu wa hali ya chini na low life class ambao ndiyo walikuwa wengi zaidi kwenye bongo Flava fan base kwa wakati huo.

Mfano, East Coast Team wao walijikita kurepresent life style fulani ya kidown-town, waliimba maisha fulani ya 'ushuani' a.k.a mboga saba. That's why ilikuwa kukiwa na mpambano kati ya ECT na Sir Nature Kiroboto, ilikuwa ni lazima Kiroboto aibuke kinara!

Huwa siisahau mwaka 2003 siku tunazindua album ya UGALI by Sir Nature. Diamond Hall ilitapika!!! Moto ulikokwa stejini, fugo la chungu likatengwa, tukapakua ugali mixa mapochopocho manjari na nyanya masaro live bila chenga!! Mpishi mkuu P Funk Majani.

Live long Sir Kiroboto. 'Hili gemu' umelitoa far away.

-Kaveli-
 
Hawezi kueleweka Sasa hivi nchi ipo uchumi wa Kati upepo umeshabadilika na nyimbo ni za kiuchumi wa kati
Wakimpa promo kama analopewa leo Jide na Clouds anajaza uwanja vizuri tu, sema Nature sio kaliba ya wasanii wa kuperform Mlimani City, yeye ni huku kwa wananchi wa dola moja per day
 
Nature ana mistari adimu pia uwezo wake wa ku ghani mashairi, lazma ukimsikiliza utacheka tu maana anaimba kihuni huni na ana represent maisha ya uswahilini typical ambayo ndio yalikuwa maisha common kwa watu wengi kitambo kile.

Nadhani majani alikuwa anainjoy ile style ya rap katuni na wepesi wa Nature kuflow ukimpa beat. Ule uswahili uswahili wa nature na uhuni uhuni ile feeling itakuwa ilikuwa inamvunja mbavu sana bila shaka tofauti na wale wasanii waliokuwa wana rep ushua ushua ambayo ndo maisha ya P.Funk toka utotoni.
 
Haujakosea. Muziki wa Juma Nature ulikuwa ni muziki wa kisela zaidi. Muziki wa kiume. Warembo wengi ule ulikuwa sio muziki wenu. Nyie enzi hizo mlikuwa mnamshobokea MB Dog, Lady Jay Dee na Mr. Paul.
Ongezea unique sisters
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…