Ni kipi kipindi bora cha asubuhi kwenye radio?

Ni kipi kipindi bora cha asubuhi kwenye radio?

Fohadi

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2020
Posts
772
Reaction score
2,421
Mara kwa mara nikiamka asubuhi huwa napenda kusikiliza radio vipindi vya asubuhi. Asilimia kubwa ya vipindi vya asubuhi vinafanana kimaudhui hapa nitachukua sample ya vipindi vitatu. JOTO LA ASUBUHI ya EFM, POWER BREAKFAST ya CLOUDS na GOOD MORNING ya WASAFI FM.

Vipindi vyote vinaundwa na watangazaji wenye majina makubwa na uzoefu katika media. Binafsi baada ya kuvisikiliza sana hivi vipindi, nimeconclude kuwa PB ni bora kwa upande wangu na Kipanya ndio ananivutia zaidi.

Tukiweka ushabiki, chuki na mahaba pembeni na ukizingatia maudhui, hoja zinazowekwa mezani na critical reasoning ya watangazaji, kipi ni kipindi bora cha asubuhi kwa upande wako?
 
Hivi kwanini kila interview anahoji ni kipanga?
 
PB n kipindi boraa ,siza, kipanya,Barbra,na kwenye magazeti Sam, wamejipangaa sana,ilaa hawa efm n 0 kwanzaa hawapeani muda wakuongea kila mtu anaropoka kivyakee,good morning wana watu wazuri ila wajipange zaidii
Tatizo GoodMorning utani mwingi na kuchekacheka sana. Inatakiwa wajipange. Angalau David Rwenyugira anajitahidi
 
Naendelea kuhesabu kura.
Wangembadili Orest Kawau aje Goodmorning angalau angeongeza kitu.
ila kule mgahawa hawapo serious...sio rahisi mtu kumsikiliza Baba levo...na ile sala yao ya jioni huwa naonaga kama mambo ya ajabu tu..anyway, ni ubunifu wao ila kwa kipindi cha jioni zamani nilikuwa shabiki wa JAHAZI enzi za Kibonde ila now nimehamia UBAONI ya EFM.
 
Naendelea kuhesabu kura.

ila kule mgahawa hawapo serious...sio rahisi mtu kumsikiliza Baba levo...na ile sala yao ya jioni huwa naonaga kama mambo ya ajabu tu..anyway, ni ubunifu wao ila kwa kipindi cha jioni zamani nilikuwa shabiki wa JAHAZI enzi za Kibonde ila now nimehamia UBAONI ya EFM.
Watangazaji wengi kwasasa hawana ‘Contents’ . Wanaunga unga sana stori za mtaani
 
Hizo redio ulizo zitaja ziko kwa ajili ya mihemeko kwanza makelele mengi yani hamnakitu hapoo mauthui ya na fanana na ujanja janja mwingi..
Hakuna redio zenye mpangilio mzuri kama hizi vipindi vya subuhi REDIO FREE AFRICA, TBC FM, REDIO ONE hawa ndio wanajua maana na maudhui ya kukupasha habari.
 
Wakati anafanya PB na Hando, Fina Mango KP alikuwa Mtu Mbad zaidi...
Hakika alikuwa mbad sana.
Fina naye anasaut flani ivi dah

Sema ile ya kuhoji ubarozi wa Denmark kipindi kile ndo ilitibua sana ya KP hadi akaamua kusepa.
 
Hakika alikuwa mbad sana.
Fina naye anasaut flani ivi dah

Sema ile ya kuhoji ubarozi wa Denmark kipindi kile ndo ilitibua sana ya KP hadi akaamua kusepa.
Ilikuaje mkuu...hebu tiririka kidogo nasisi tuzifahamu enzi
 
AMKA NA BBC
Hii huwa sipendi kuikosa, mi nasikiliza radio kutumia online huwa natumia radio one kuipata sasa siku wakiwa offline na muda ndio umefika nitaanza kuisaka amka na bbc kwenye viredio vyote hadi niipate, kuna siku niliifuma kwizera fm, nikiwa bongo huwa nasikiliza radio one saa kumi nambili kamili hadi saa moja na robo, nahamia clouds hadi wamalize uchambuzi wa magazeti baada ya hapo sisikilizi redio tena hadi saa tatu usiku sports extra, kule namfata kiemba
 
Back
Top Bottom