Ni kipi kipindi bora cha asubuhi kwenye radio?

Ni kipi kipindi bora cha asubuhi kwenye radio?

Hakika alikuwa mbad sana.
Fina naye anasaut flani ivi dah

Sema ile ya kuhoji ubarozi wa Denmark kipindi kile ndo ilitibua sana ya KP hadi akaamua kusepa.
Fina alikuwa ana sauti na Lugha ya Ki Malkia nzuri sana...

Hivi ile Issue ya KP na Fina Kusepa walikubaliana wote na Hando then Hando akawasaliti ilikuwa ni kuhusu MIC zilivyowazingua baada ya ugeni kutoka Denmark au nachanganya?
 
Fina alikuwa ana sauti na Lugha ya Ki Malkia nzuri sana...

Hivi ile Issue ya KP na Fina Kusepa walikubaliana wote na Hando then Hando akawasaliti ilikuwa ni kuhusu MIC zilivyowazingua baada ya ugeni kutoka Denmark au nachanganya?
Kwani Barbara kaanza kuwa kuwa kwenye PB mwaka gani...maana naona mnamtaja Mango sana.
 
Ilikuaje mkuu...hebu tiririka kidogo nasisi tuzifahamu enzi
Timu ya breakfast ikiongozwa na Kipanya , Fina.
Walikuwa na miadi ya kuhoji baloz wa Denmark hapa nchini ktk ofisi yake.

Kuna vitu flani flani walienda kuhoji.

Jamana mwenye kuongezea aje asimulie hahaha😀😀

Kulitokea sintofaham yale mahojiano hayakwenda hewani.

Nadhani walitibuana baina ya KP na Uongozi wa Clouds media

Kp akafukuzwa kazi.

Lakini baaaaaaaaaaaadaye
Walimrudisha.

Ndo maana Masoud Kipanya kapunguza utu mbad
Nahisi walimuomba msamaha ndo maana akarudi

😀😀😀
 
Power Breakfast

Ila mimi nilikuwaga nafuatilia kipindi kile cha Barbara Hassan, Gerald Hando na PJ sijui kama hadi leo bado wanasemaga hivyo
 
Fina alikuwa ana sauti na Lugha ya Ki Malkia nzuri sana...

Hivi ile Issue ya KP na Fina Kusepa walikubaliana wote na Hando then Hando akawasaliti ilikuwa ni kuhusu MIC zilivyowazingua baada ya ugeni kutoka Denmark au nachanganya?
Hando alirudi nyuma

Ila Kp na Fina hawakurudi nyuma
Walichukua barua zao za kuachishwa kazi wakasepa.

Kp nilimsikia siku moja akisema kuwa hakuwai hata siku moja kupewa barua ya Onyo kipindi cha utumishi wake pale Clouds.
 
Power Beak fast ya Clouds ni kipindi bora kwa sasa. Good morning ya wasafi watangazaji wengi alafu masihara mengi, hapo Zembwela na zungu hawakupaswa kuwepo, kwenye usomaji wa magazeti abaki kienge peke yake Host wa kipindi abaki David na yule Dada E fm wajipange sana bado mno
 
Hii huwa sipendi kuikosa, mi nasikiliza radio kutumia online huwa natumia radio one kuipata sasa siku wakiwa offline na muda ndio umefika nitaanza kuisaka amka na bbc kwenye viredio vyote hadi niipate, kuna siku niliifuma kwizera fm, nikiwa bongo huwa nasikiliza radio one saa kumi nambili kamili hadi saa moja na robo, nahamia clouds hadi wamalize uchambuzi wa magazeti baada ya hapo sisikilizi redio tena hadi saa tatu usiku sports extra, kule namfata kiemba
Mie amka na BBC ikishapita sipati nafasi ya kusikiliza radio labda jioni kwenye daladala.
 
EA radio wako bora zaidi, wanacover issue zote serious, japo Mashauri sijajua kama anaongea sana au kuna issue irrellevant anaziongelea (something inapitiliza, too much boosting may be). Clouds wako poa ila matangazo nayo yamezidi japo siku hizi nakuwa EA radio asubuhi na jioni niko kwenye ndinga.
 
Pb wako vizuri sana efm eti kingwendu nae eti ni mtangazaji [emoji35][emoji35] yani nikae nimsikilize kingwendu anipe madini aisee ni utani huu
 
PB imejipambanua vizuri kabisa, kila mmoja ana role yake na anaimudu vizuri. Barbara ni Host mzuri kabisa, KP & Cza ni wachambuzi wanaochambua mambo kwa kina.

Sam anamudu vizuri usomaji wa magazeti kwa mtindo wa kipekee unaovutia masikio ya msikilizaji.

Bonge naye nafasi yake anaimudu vizuri jambo ambalo wanajikuta wanatengeneza timu moja hatari sana yaani akikosekana mmoja unaona kabisa kuna pengo.

Napenda sana pia segments zao zimepangiliwa vizuri sana ingawa huwa navutiwa zaidi na magazeti kutokana na namna Sam, KP na Cza wanavyoungana kuchambua mambo.

Huwa sifurahii kipindi Fredwaa akiwepo, sielewagi position yake pale CMG. Ila kwangu PB ya Clouds FM ipo juu sana na haina mpinzani kwenye shows za asubuhi kwenye redio za Tanzania.
 
Yani mtazamo wako Na wangu uko sawa kabisa kwa mm segment ya magazeti ndio huwa naikubali zaidi
 
Back
Top Bottom