Ni kipi kipindi bora cha asubuhi kwenye radio?

PB is the best. Combo moja matata Sana la barbara H na Kipanya , siza na sasali na Bonge ila Fredwaa nadhani wangempumzisha. Huwa anaharibu chemistry.

Zamani Kipanya na Fina walinoga zaidi na Hando.

Kwenye TV clouds barbie na PJ wamebond vizuri sana asubuhi halafu content ya kushiba. Hongera kwa Director and producer na watu wote behind the scene maana Bila hawa tusingepata kilicho bora.

Swali fikirishi mbona tv za kenya kama Citizen,Ktn,ntv asubuhi zina content nzuri yaani interview kuliko za bongo. Mfano sasahivi sintofahamu angeletwa waziri wa habari atueleze hali ya mweshimiwa akapigwa maswali lakini waandishi wetu hawaendi na uhalisia.
 

umemaliza kila kitu mkuu.
Yaani fredwaa anakuwaga kama anajishtukia Fulani hivi yuko hewani hewani. Chemistry ilikataa kabisa kuungana na wenzake labda angepewa pindi jingine
 

hata vipindi vyao katika tv ni vizuri kuliko vipindi vya tv tanzania. redio zao wanavipindi vizuri kuliko tz kenya wapo vizuri
 
Daah kama Mimi..Ubaoni ndo kila kitu,Imma Kapanga,Roman Shirima na Mpoki,,Traffic Jam siielewi
 
Ukiwa na uwezo wa kazi utafuatwa tu! alipoondoka Masoud Clouds kwenye PB walipwaya sana

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Radio free afrika ....Amka na BBC na kipindi Cha magazeti kila siku asubuhi lazima nianze siku namna hiyo
Mie pia naanza na amka na BBC naunganisha na magazeti ikifika saa moja nahamia clouds
 
Kwa PB bado hujanishawishi, akina Kipanya wako gado sanaa.
 
Well said mkuu... Vipi kipindi cha Leo tena? Huwa wananivutia sanaa, hasa kipindi akiwepo yule Musa kama sikosei kwenye ile timu yao.
 
Hakuna kitu kama hicho kwa sababu zifuatazo:-
1: Ifahamike kwamba kuna tofauti kubwa programe za asubuhi na jioni, MF kipindi cha asbh cha Radio 1 kilifaa kuwa jioni kwani wao wanaongelea mada zaidi na ndiyo maana wachangiaji wa simu ni wengi kwani jioni ni muda ambao watu wametoka kazini, wamepumzika nk. Tofauti na asubuhi ambapo Mara nyingi ni muda ambao hakuna mtu mwenye muda wa kupiga simu, ila ni muda ambao mtu anahitaji kupata habari na mambo yaliyojiri kwa wakati huo (Current story) na ndicho wanakifanya PB (Hongera kwao kwa ubunifu huo?

2: Utangazaji wa sasa ni modern si kama zamani, yaani media zinatakiwa kuwa na watu wenye ubunifu na zaidi ufahamu wa kuchambua mambo nyeti kulingana na nyakati, , , , kama utakumbuka ndani ya PB zamani kulikuwa na Segment inaitwa Jicho la Ng'ombe ilikuwa inaonesha ukosowaji wa moja kwa moja kwa njia ya mafumbo kwa serikali ila waliishtia na kuifuta hiyo segment, baadaye wakaleta kitu kinaitwa Kuperuzi na Kudadisi(Kwa sasa ni Kudonoa na Kudadisi) baada ya serikali kukataza media kusoma story kwenye magazeti na badala yake ikawa ni Headlines tu, wakamleta Sasali kwa kazi hiyo na bilashaka anaifanya vema kuliko PJ alivokuwa akifanya hapo kabla.

3: Kwa idadi ya watu kwenye vipindi hasa asbh na jioni karibu media zote kwa sasa ziko sawa kwani ni ngumu kipindi cha Massa 3/4 afanye mtu mmoja au wawili, ukweli ni kwamba Audience wanahitaji ladha tofauti masikioni, , , , hapo media zote ziko sawa.

4; Mwisho ni kwamba utangazaji siyo kuongea tu kwenye Mic, Bali uwezo wa kufikiri, kuchambua, ku- challenge nk, , , Nisem Clouds wamejitahidi kwa hilo ingawa Radio 1, E FM na Wasafi wanawatangazi wazuri lkn huwezi walinganisha uwezo wao na Kipanya, Cza, au Sasali, , , ,

Kama huyu Kitenge wakati yupo IPP alikuwa na akili lkn tangu aende Wasafi anaropoka ropoka tu studio na mwenzake Zembwela utadhani wanapita mtaroni[emoji3] wakati naye akiwa East Africa alikuwa timamu, Na huyu Mwaipaya sijui nani ndo hata hana kitu wao asbh asbh simu na mada za Ndoa kila siku kama vile wahubiri wakati kuna mambo nyeti ya kuzungumzia.

Sasa hawa niliowataja utaweza kulinhanisha uwezo wao na Kipanya, Cza au Sasali?
Yaani fikiria Kitenge, Zembela au Mwaipaya afanye Interview na Prof Lipumba, Zitto, Lissu, Majaliwa (wataishia kucheka tu)[emoji23]

Kwangu PB ni Bora zaidi!
 
PB n kipindi boraa ,siza, kipanya,Barbra,na kwenye magazeti Sam, wamejipangaa sana,ilaa hawa efm n 0 kwanzaa hawapeani muda wakuongea kila mtu anaropoka kivyakee,good morning wana watu wazuri ila wajipange zaidii
True ila kipindi kile yupo gerald hando na pemben paul james pj na barbara hassan na ciza aisee kipindi kilikuwa hot sana masudi naona anapooza sana
 
Sala ipi mkuu maana mi sijawahi kusikia kipind hicho ni sala ipi?
 
Power Breakfast

Ila mimi nilikuwaga nafuatilia kipindi kile cha Barbara Hassan, Gerald Hando na PJ sijui kama hadi leo bado wanasemaga hivyo
Hapa hata mimi niliwakubari kinoma walifit kisawasawa, masudi mi naona kapooza sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…