Teamo
JF-Expert Member
- Jan 9, 2009
- 12,271
- 1,052
..............Kwamba hizi shughuli maarufu kwa jina la 'SHEREHE YA JIKONI' zinazidi kuchukua sura mpya,na pengine KUPOTEZA MAANA,au mimi ndio sijui maana.Ndio maana nimeamua KUISTIPULATE ISHU HAPA!
katikati ya 'shughuli' nimesikia jana kipengele kinaitwa MADA,nikiwa katika mojawapo ya maeneo yangu ya kujidai pande za kimara.Kwa namna walivyokuwa wakimshauri bibi harusiu mtarajiwa UKWELI HAIKUWA SHEREHE YA JIKONI ambayo pendine ufahamu wangu mdogo ulinidadavulia ki vile.Mama zetu walikuwa wakijadili mambo ya CHUMBANI tena kwa kina sana,na katika sehemu ya halaiki,tena muda ulikuwa bado kabisa.
Sasa mimi nilikuwa nafikiri labda hizi sherehe zingetofautishwa siku kwa kuzingatia MAADILI,na umaana wenyewe.hii itasaidia 'wadau' wa sherehe hizo kuzitafutia muda muafaka,eneo stahili na pengine kukinusuru kizazi kinachofuata kusikiliza 'mambo ya chumbani' moja kwa moja kutoka kwenye vinywa vya wazazi wao.
Au ninakosea wadau?