Ni kitendo gani au tukio gani usilolisahau lililobadilisha maisha yako?

Ni kitendo gani au tukio gani usilolisahau lililobadilisha maisha yako?

Fohadi

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2020
Posts
774
Reaction score
2,439
Kila mtu kwenye maisha nina amini ana turning point yake. Turning point ni sehemu au pointi ambayo ilibadilisha maisha yako. Inaweza ikawa ni tukio, safari, kukutana na mtu au jambo lolote ambalo kwa namna moja ama nyingine limekufanya uwe hapo leo either kukupandisha au kukushusha kimaisha.

Naomba nieleweke kabisa kuwa sio lazima yawe ni mafanikio makubwa sana ya kumiliki mali nyingi za thamani au matatizo makubwa sana yanayokukumba leo. Hapo ulipo leo (Juu au chini kimaisha) hakujatokea kwa bahati mbaya, kuna kitu kilitokea ambacho kimefanya ukawa hivyo leo. Ni kitu gani hicho?, naomba share nasisi ili tujifunze kupitia makosa au ubunifu wako na kupata uzoefu zaidi.

Naanza mimi:

Sitaisahau safari niliyoifanya alfajiri ya tarehe 9 january miaka mingi iliyopita ambapo nilikuwa natoka mkoani na kuja Jijini Dar. Ile safari imenifungulia dunia. Kuja kwangu Dar ndio ilikuwa turning point ya maisha yangu maana kule mkoani nilikuwa sina 'direction' ila Dar imenifungulia fursa nyingi sana.

Simaanishi nimefanikiwa, hapana! ila naiona tofauti kubwa iliyopo kati ya Fohadi wa miaka ile na huyu wa sasa aliyeweka mazi ya kudumu Dar.

Simaanishi kuwa sitatoka Dar, hapana, nitatoka dar nikipata fursa sehemu nyingine ila bado safari ya kuja Dar ndio iliyobadili maisha yangu kabisaa.

Kila mwaka huwa naikumbuka 9 January maana ndio siku nilipofanya hii safari ya matumaini na bila shaka tarehe 9 january ni birthday ya mafanikio yangu ya leo na ambayo nitayapata kesho panapo majaaliwa yake Mwenyezi.

Wewe unakumbuka nini? Tukio au kitu gani kimebadili maisha yako.

Karibuni.
​
 
Back
Top Bottom