Ni kitu gani ambacho kiliwahi kukutoa ushamba?

Ni kitu gani ambacho kiliwahi kukutoa ushamba?

Aisee nakumbuka zamani Sana,tulikuwa lodge na boyfriend wangu. Tulikuwa tuna safiri,katika kufukunyua fukunyua nikaiona laptop ya babe kwenye begi lake,nikaichukua. Nikaona kitufe cha power,nikaiwasha. Nikasikia raha mwenyewe kuichezea laptop kwa Mara ya kwanza,Maana Nilikuwa Naiona ona tu kwa watu. Baada ya muda nikamsikia babe alikuwa anaongea na simu nje,anarudi chumbani kwetu. Nikazima pale kwenye power nikairudishia.
Babe alivyoingia akasema ngoja tucheck movie,akaitoa laptop. Akaniambia sasa mbona hujaizima?? Nikakataa sijaishika wala kuichezea. Alicheka Sana mpaka machozi yakamtoka,alinicheka mpaka nikakasirika. Akanionyesha vile vitaa pale vilivyoongozana vya chaji na vitaa vingine. Akaiwasha halafu akaniambia ukitaka kuizima unafanya hivi.
Aisee Hadi niliacha kununa nikajikuta nacheka tu mwenyewe,nikakiri kweli niliiwasha.
Aisee laptop iliniaibisha Sana sitosahau.
Mimi ilikuwa pc ya mshkaj halaf nikajitia much know huhuhuhuhu aibu ya mwaka the same with u
 
Kwa mala ya kwanza nimeingia mjini nikitokea kijijini niliko zoea kula ugali mkubwa wa kusaza maziwa jumlisha michembe na numbu za kusombelea walio wahi kukaa kijijini mtanielewa zaid.Nilifika mjini mida ya jioni sana.Kasheshe ilikuja wakati wa msosi usiku naona zinapakuliwa ndizi nakuhifadhiwa kwenye ile kitu mnaita hotpot baada ya hapo ikawekwa mezani then nikaona kilamtu anachukua mule anaweka kwenye sahani yake anakaa kwenye kochi nakuanza kula nikawaza ndotunakulaa ama nikama kibuludisho kwa mgeni kwasababu sikuamini kama zilendizi zilizopikwa zinaweza kuwa chakula cha usiku maana ningeweza kuzila zilendizi zote nakuzimaliza bila kushiba.Bas zamuyangu ikafika nikachukua sahani wakawa wananishangaa maana nilichukua za kutosha nikala zikaisha badae naona watu wanaingia kulala ohooo nikaanza kupata wazo kuwa inawezekana nimsosi wa usiku kweli bado nilikuwa sjaamini sababu baba yangu mdogo ambae ndo mwenyejiwangu mkuu alikuwa hajaludi toka kazini alipo lud akamwambia mkewe mgeni amekula akajibu ndio huku mimi nikiskia kauli hiyo ndonikaamini kuwa tayali baba aliniita nakuniuliza kama nimekula nikamwambia ndio ila naskia njaa balaa ikabid nipikiwe ugali mkubwa usiku huo.nyumbanzima nilionekana wa ajabu
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Je nikitu gani ambacho kiliwai kukutoa ushamba katika maisha yko unacho kikumbuka..

Mimi ni pikipiki ilinitoa ushamba sana hicho kitu enzi hizo lakin
weka na chako twende sawa
Nilipo jipigia bao siku ya kwanza usiku, asubhi nilimwonyesha mama kuwa nimejikojorea mkojo mzito
 
Simu yangu ya kwanza kumiliki ilikuwa Alkatel, siku tatu za mwanzo sikuwahi kuiona iki vibrate.
The other day nilikuwa naendesha baiskeli simu nikatumbukiza kwenye back pack, sijui ilijibonyeza vipi ikaita kwa vibration, kitu ambacho nilikuwa sijakitegemea kabisa.
Nikajua ntakuwa nimebeba panya au snake kabisa. Niliruka kama ninja baiskeli ikadondokea chaka lingine mimi kwenye vumbi, begi nalo nimetupia mbali kabisa..
Nikatafuta bonge la fimbo nikaanza kutoa kichapo kwa lile begi hadi niliporidhika chochote kilichomo kitakuwa kimeshakufa.
Kuja kufungua begi duuh!! simu haifai. Nilitamani kwenda kujishtaki polisi mwenyewe
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] nimeipenda nataman ningekuepo
 
Enzi hizo kitega uchumi ndio habari ya mjini ground floor palikuwa na restaurant, tumeenda na mwenyeji wangu katika kujihudumia nikachukua sahani nikaweka sambusa, yai la kuchemsha na eggchop bila kujua kwamba ndani kuna yai, wakati wa kula nashangaa nakutana na yai, nikajikausha.
 
Back
Top Bottom