Ni kitu gani hasa kinachofanya hizi tume ziitwe "Tume Huru"? Uhuru wake ni upi hasa?

Ni kitu gani hasa kinachofanya hizi tume ziitwe "Tume Huru"? Uhuru wake ni upi hasa?

Hivi mbona kauli ya "nywi nywi nywi" hajawaambia wachunguze!!🤔🤔
 
"Tume Huru ya uchaguzi imemaliza kazi yake siku chache tu zilizopita na matokeo yake tumeyaona.

Sasa kumeundwa "Tume Huru" nyingine ya kuchunguza mambo ambayo kila mtu mwenye akili timamu anajuwa sababu zake na matukio yaliyo ambatana na sababu hizo.

Kwa nini pawepo na matarajio tofauti na yale ya "Tume Huru" iliyo bariki chanzo cha haya matukio yatakayo chunguzwa na hii tume mpya iliyoundwa?

Ni kitu gani hasa kinachofanya hizi tume ziitwe "Tume Huru"? Uhuru wake ni upi hasa?

Kwa nini Samia Suluhu Hassan anapenda sana ulaghai na kejeli za aina hii? Huwa haoni kuwa waTanzania wanajuwa maana ya "Tume Huru" ni kitu gani?
Unaambiwa 'form four' alipata leaving certificate tuu hakupata academic certificate.....
 
Njaa, kujikomba au uoga wa kudogoshwa ndio kuna waponza, huenda she's offering a heavy amount au wanna lipa favor.
"Njaa"? Hapana.

Maana ya kwamba kati ya wote hao walio teuliwa kuna hata mmoja atakosa kutimiza mahitaji muhimu?

NNaamini kwa dhati kabisa kwamba kitu muhimu sana kinacho kosekana miongoni mwa waTanzania ni kuweka maslahi ya nchi hii mbele zaidi ya kitu kingine chochote.

Wengi wa hawa wateuliwa kwenye hiyo timu watakuwa na visababu binafsi zaidi kuliko ustawi wa taifa lao. "Njaa" inaweza kuwa ni kisingizio tu, kisababu kidogo sana miongoni mwa sababu nyinginezo ambazo hawawezi kuziweka bayana. Imani ni mojawapo.
 
Unaambiwa 'form four' alipata leaving certificate tuu hakupata academic certificate.....
Lakini si anao wasaidizi wenye madigrii ya kila namna, hawa watu kwa nini wanajiweka kwenye hali ya uduni kiasi hiki?

Si hivyo tu, hatua zilizomfikisha hapo huyu mtu asiyekuwa na kitu kichwani ndizo mbovu kabisa!
 
Back
Top Bottom