Ni kitu gani hupelekea vijana wengi kuwaombea wazazi wao wafe ili warithi na kuuza mali?

Mboka man

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2020
Posts
478
Reaction score
1,647
Japo sio vijana ila vijana wengi sasa hivi ambao wazazi wao wamebahatika kuwa na Mali kila iendayo leo wanaombea wazazi wao waondoke hapa duniani ili waweze kurithi Mali na kuuza Mali.

Wako wengine wazazi licha wako Hai tayali wameshapiga hesabu wako wangapi kwa baba yao, wameshapiga hesabu hii nyumba tukiuza tugawane ngapi ngapiii hivyo kila iendapo leo wanapiga hesabu hawa wazee wataondoka lini yaani kila kukicha wanawaombea wafe.

Je, tatizo ni nini mpaka vijana wanapelekea kuwa na haya mawazo ni kwanini wasitafute vya kwao.
 
Ukimuambia kijana atafute Mali zake bila kumuandalia mifumo sahihi ya yeye kufanikiwa huo ndo Mwanzo wa Matatizo.

Kama mzazi unabidi kumpatia mtoto Mali za yeye Kuanzia Maisha.

Unapozaa mtoto Hilo ni jukumu lako la kuhakikisha unampa Maisha Bora ikiwemo kumpa Mali na mtaji na Elimu Bora yenye future.

Kama unaona hauna Cha kumpa au kuwapa watoto wako usijiaumbue kuzaa maana watoto watateseka Bure. Na watakuua au kukuombea kifo.

Dunia ya leo sio kuzaa mtoto bila mipangilio maana kuwa na watoto wengi masikini wanaofanya Kazi za kitumwa za kulipwa ujira Mdogo viwandani na ukuli Mtu wa hivi atakuua au kukuombea kifo.
 
Ukimuambia kijana atafute Mali zake bila kumuandalia mifumo sahihi ya yeye kufanikiwa huo ndo Mwanzo wa Matatizo

Kama mzazi unabidi kumpatia mtoto Mali za yeye Kuanzia Maisha .

Unapozaa mtoto Hilo ni jukumu lako la kuhakikisha unampa Maisha Bora ikiwemo kumpa Mali na mtaji na Elimu Bora yenye future

Kama unaona hauna Cha kumpa au kuwapa watoto wako usijiaumbue kuzaa maana watoto watateseka Bure. Na watakuua au kukuombea kifo.

Dunia ya leo sio kuzaa mtoto bila mipangilio maana kuwa na watoto wengi masikini wanaofanya Kazi za kitumwa za kulipwa ujira Mdogo viwandani na ukuli Mtu wa hivi atakuua au kukuombea kifo
Tunapo sema mzazi kumpa mtoto wake mali/mtaji, wewe unaitafsiri vipi??
 
Umpe mtoto Mali aanzie maisha kwa mipango ipi?

Mtoto atafute za kwake..
 
We jamaa acha mawazo ya kuua wazazi wako. Kwa uandishi wako ni kama unapima upepo juu ya adhma mbaya ulo nayo. Sikia, hata baada ya kuwa ua hutakaa ufurahie manisha na kuna uwezekano utaanza wewe kufa au kifungwa.
 
Tunapo sema mzazi kumpa mtoto wake mali/mtaji, wewe unaitafsiri vipi??
Atafute Mali zake,,
.kitendo cha kumpa sehem ya pesa akaanzishe biashara ni kuzidi kujitafutia matatizo,

Kumbuka pesa yeyote usiyoitolea jasho huna uchungu nayo.

Nimeona watu wamepewa pesa kibao na wazazi wao wafanye maisha,
Wameishia kuhonga pesa zote na bado anarudi kwa baba kulialia apewe zingine,,

Dawa akatafute za kwake.

Kama mzazi uliweza ukatafuta zako Bila msaada wa baba yako kwann yeye asiweze tafuta?
 
Mumeyalea kama wali Boko Boko acha wawanyooshe.

Mimi toto langu haliwezi.kulelewa kienyeji,kama nilivyolelewa na Mzee kwamba Sina changu na matoto yangu nitalea hivyo hivyo
 
Atafute Mali zake,,
.kitendo cha kumpa sehem ya pesa akaanzishe biashara ni kuzidi kujitafutia matatizo,

Kumbuka pesa yeyote usiyoitolea jasho huna uchungu nayo.

Nimeona watu wamepewa pesa kibao na wazazi wao wafanye maisha,
Wameishia kuhonga pesa zote na bado anarudi kwa baba kulialia apewe zingine,,

Dawa akatafute za kwake.

Kama mzazi uliweza ukatafuta zako Bila msaada wa baba yako kwann yeye asiweze tafuta?
Ndo maana mnauliwa na watoto wenu ,kwanini unazaa mtoto na hauna Mali za kumpa ? Ubinafsi ni hatari Sana kwa ustawi wa jamii
 
Umpe mtoto Mali aanzie maisha kwa mipango ipi?

Mtoto atafute za kwake..
Akatafute wapi then hii issue ya watu kuua wazazi hipo kwa wazazi wenye mitazamo Kama yako unapomwambia kijana akatafute Mali zake bila kumpa Elimu Bora na mtaji unadhani anatoboaje ebu waangalie vijana wa uswahilini !
 
Ukimuambia kijana atafute Mali zake bila kumuandalia mifumo sahihi ya yeye kufanikiwa huo ndo Mwanzo wa Matatizo

Kama mzazi unabidi kumpatia mtoto Mali za yeye Kuanzia Maisha .

Unapozaa mtoto Hilo ni jukumu lako la kuhakikisha unampa Maisha Bora ikiwemo kumpa Mali na mtaji na Elimu Bora yenye future

Kama unaona hauna Cha kumpa au kuwapa watoto wako usijiaumbue kuzaa maana watoto watateseka Bure. Na watakuua au kukuombea kifo.

Dunia ya leo sio kuzaa mtoto bila mipangilio maana kuwa na watoto wengi masikini wanaofanya Kazi za kitumwa za kulipwa ujira Mdogo viwandani na ukuli Mtu wa hivi atakuua au kukuombea kifo
Nakuhakikishia ukiwa na mentality ya namna hii kwa mtoto/watoto wako utaumia mnooo, wazazi wanawajibika kuwalea watoto vizuri, kuwapa elimu nzuri na kufundisha kujitegemea, sio kwaandalia "utajiri"

Mungu anawapa watoto vipawa tofauti tofauti, jukumu la mzazi ni kuvitambua n'a kuvipalilia mtoto angali mdogo, akifikisha umri wa kujitegemea, mwache akajitegemee, tena usimhurumie hurumie hata kidogo, maana ukifanya hivyo utaua creativity yake.

Waambie watoto wako, mali uliyochuma wewe na mama yao, ni ya kwako na mama yao, wao wajibiishe kutafuta vya kwao pia, hata kama umewaandalia assets kadhaa, but usiwaambie mapema, watabweteka! Acha waijitafute kwa bidii itafungua milango mingi kwenye maisha yao.

Ni ushauri na mtazamo wangu tu.
 
Back
Top Bottom