Ni kitu gani kimekusukuma kufanya ujenzi?

Ni kitu gani kimekusukuma kufanya ujenzi?

Fibanochi

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2018
Posts
476
Reaction score
1,018
Habari za majukumu mabibi na mabwana!

Katika harakati hizi za maisha watu hupitia mengi sana, Kuna kipindi pesa inakubali, Kuna kipindi unachapika mpaka unajuta kuzaliwa. Anyways twende kwenye jambo la msingi, hivi ulisukumwa na na nini mpaka kufikia uamuzi wa kujenga nyumba unayoishi? Ni dhahiri kabisa kwa walio wengi watakwambia walichoka na usumbufu wa ma baba na mama wenye nyumba zao.

Binafsi nimepanga kwa miaka lukuki na nimekuwa nilibadilisha maeneo mengi jijini, nimeishi Sinza, Magomeni, K'nyama, Ilala na Kinyerezi. Kwasasa ndiyo nimeanza ujenzi na nipo katika hatua ya kupaua, ni nyumba yangu ya kwanza.

Kitu kilichonisukuma kufanya ujenzi ukiondoa adha za wenye nyumba, ni kile kipindi nazunguka na madalali kuangalia nyumba, alafu unakuta nyumba miyeyusho tu au ya kawaida tu kisha kodi kuuubwa, unakuta unajiuuliza hivi me nikiamua kujipinda kweli siwezi jenga nyumba kama hii au zaidi ya hii kweli? Lakini kingine ni ile hali ya kutaka kukaa sehemu nzr, kupata amani ya moyo na kufanya mpangilio wa kila unachotaka.

Embu share nasi, ulisukumwa na nini kujenga nyumba yako ya kwanza ya kuishi?
 
Mimi kinachonisukuma kipo kabisa,ila sasa ela ya kusindikizia huo msukumo ili nianze ujenzi kama wewe ndo bado sijapata!
Acha niendelee kusukumwa huku nikisubiri ela alafu nikianza ujenzi ntakupa mrejesho msukumo wangu ulisababishwa na nini!
 
Mke wangu ana gubu, na dharau,anatunishiana misuli na wenye nyumba,yaani kila nyumba tukipanga ile kodi ya kuigilia ndio huwa ya mwisho.

Tukaona tujenge ya kwetu/ zetu.sasa hivi nae ni land lord na upole umekuja ghafla.
Nae eti anachukia wapangaji wakorofi.
 
Mimi kilichonisukuma ni hiki kipindi fulani baada ya kupigika kweli mtaani baada ya kumaliza chuo nilianzisha bissines fulani ya mafuta ya kula .

biz ikachanganya kwa namna fulani kuna wakti nikafunga mzigo kaa wa dumu ishirini hivi huku dumu moja likiwa 70,000/-tsh nikiwa katika haraka za kutaka kuanza kuziuza , kuna mambo fulani yakatoka yaliyopelekea nishindwe kufanya biashara kwa miezi kama minne hivi .

Nakuja kurudi kwenye biashara nakuta b dumu limepanda limefika 100,000/= baada ya kusukuma mzigo ulipoisha nikajikuta kweli pesa inaonekana nikaona mmmmhh !! Hizi zisije nishinda nguvu nikaanza kutumia kuonga mademu pamoja na pombe nikajisemea acha nijitose tu kujenga , hivi sasa napiga hesabu ya namna ya kupiga bati .
 
Mke wangu ana gubu, na dharau,anatunishiana misuli na wenye nyumba,yaani kila nyumba tukipanga ile kodi ya kuigilia ndio huwa ya mwisho.

Tukaona tujenge ya kwetu/ zetu.sasa hivi nae ni land lord na upole umekuja ghafla.
Nae eti anachukia wapangaji wakorofi.
Hahhahahaha nimecheka kwa sauti lkn bora alikuchachafya ukachoka kuama kila miezi sita if not kumi na sasa mna kwenu
 
Kodi kubwa, wengine tuna vitu kibao kuhama tu ni mtihani hadi ukodi fuso na baadhi ya vitu kuharibika kwenye process ya kuhama......kupewa taarifa za kukumbushiwa kodi tunahisi kudhalilika, maneno ya hovyo hovyo kutoka kwa wapangishaji wengine hasa akina mama.
 
Hahhahahaha nimecheka kwa sauti lkn bora alikuchachafya ukachoka kuama kila miezi sita if not kumi na sasa mna kwenu
[emoji28][emoji28][emoji119][emoji119],unakuta fenicha zinachakaa mapema kwa kuhamisha hamisha,pilika pilika vioo vya makabati vinavunjika, baadhi ya vitu vinapotea,kukutana na watu wa mitaa kila mtu na tabia zake, kila miezi sita wewe ni mgeni mtaa mwingine[emoji28][emoji28]
 
Hahahahaha ila jaman kuna wenye nyumba kichefuchefu, yani hata kama hutaki shari kwake lazima uipate
 
Hahahahaha ila jaman kuna wenye nyumba kichefuchefu, yani hata kama hutaki shari kwake lazima uipate
Sasa wakikutana na muhaya wangu ,vinaumana,dharau,kujikweza,shombo zote mdomoni zipo,[emoji28][emoji28][emoji119][emoji119]
Mwisho wa siku mwenye nyumba anachemka utasikia, " kodi yenu ikiisha muhame, sipokei tena kodi kutoka kwenu"
 
Back
Top Bottom