Ni kitu gani kinakufanya ujue “Restaurant” bei yake sio za kitoto

Ni kitu gani kinakufanya ujue “Restaurant” bei yake sio za kitoto

Wengine wahudumu ni wezi naongelea hizi pub za kawaida kama juliana.

Siku moja tupo juliana mtu kama sita. Agiza jb, absolute vodka, kiti moto, soda za kumwaga ili mradi tulifanya fujo! Yule mhudumu si kaleta bili laki tisa!

Tukamwambia poa utaifuata! Kuja kufanya ujasusi kinywaji cha elf 60 ye anaweka laki! Yaani anaiba elf 40 per drink.
 
Kuna restaurant niliwahi kwenda Masaki kufika tu mnafunguliwa mlango na mzigo mnapokewa nikajiambia tu bora nilibeba kadi yangu ya benki ingekuwa fedhea 😂

Pale Hyatt ni hoteli lakin wanakufungulia hadi mlango wa gari.

Mdau wewe Ni kitu gani ukikikuta kwenye mgahawa unajua bei lazima itakutoa jasho??
Hyatt mbona Buffee ni Jiwe tu hakuna maajabu.
 
Back
Top Bottom