Ni kitu gani kinakufanya ujue “Restaurant” bei yake sio za kitoto

Ukiona kuna kamziki kalaini na watu hawaimbi kwenye hiyo nyimbo kwa kifupi ni beat ya taratibu tu bila kuskia maneno sepaa. Au ukiskia haya maneno starter, main course, salad course na dessert we tangulia nje.
 
Kuna siku niliitwa na mchuchu sehemu nikajua hapa hapa pamechangamka mapema, ikabidi kwanza nitambue bei za pale maana sikupanga kuwa na matumizi ya zaidi ya fedha niliyo enda nayo
 
Ukifika restaurant ukaagiza chakula wanakuambia wanakwenda kukitengeneza dakika arobaini, halafu bill inaletwa kwenye hard cover Kama ya kitabu. Jiandae na wekundu wa kutosha.
Kuna mahala downtown niliagiza kahawa,wanatengeneza nawaona,. wakaleta style hizi,bill imeletwa kwenye kitabu cheusi,.nilienda kulilia home..nilisonya njia nzima.. binti kiziwi ,ungekuja kunigomboa??
 
Nikiwa nimerudi nchini wakati huo toka mashariki ya kati, siku moja nikaingia kwenye restaurant moja pale Victoria inaitwa Kyana khazana
Kuingia tu pale ndani mazingira yake yakanianimbia hapa nijiandae.. Basi akaja mhudumu mmoja nadhifu sana kaniletea menu
Nikiri wazi baada ya kuisoma menu yote nilichoweza kuagiza ni portion ya matunda sh.5000 nikakisemea hayo nitashiba
lahaula Rasuri 😭 nilicholetewa ni kabakuli ka vipande vya embe, parachichi ndizi na tikiti.. Huku mtaani ukiuziwa jero unaweza kupigana😂
Nikakaza roho nikala nikaitisha bili ikaletwa kwenye kisahani lilichowekwa kijitabu huu yake.. Nikajua leo shughuli ipo
Kufunua kale kakitabu jumla ilikiwa 7500😂 5000 matunda, 1000 service chaji 1500 kodi... Nilihisi homa ya ghafla ila nikajikaza nikalipa nikasepa😂😂😂 huwa sipasahau pale mahali..ila siku hizi pamevunjwa
 
Eneo la mgahawa ulipo ndio ishara #1. Oyster Bay na Masaki kwa Dar es Salaam ni rahisi sana kupata migahawa ya gharama kubwa ukilinganisha na maeneo mengine. Ssb kuu hayo ni maeneo yanayokaliwa na wageni wengi waliopo kikazi nchini ukijumlisha na wazawa wachache wenye vipato vikubwa. Migahawa kama Epi d'or na Karambezi haiwezi ku-survive Tandalale, Mbagala, Tabata, Buguruni, Sinza n.k
 
Kuna mahala downtown niliagiza kahawa,wanatengeneza nawaona,. wakaleta style hizi,bill imeletwa kwenye kitabu cheusi,.nilienda kulilia home..nilisonya njia nzima.. binti kiziwi ,ungekuja kunigomboa??
Always always! isipokuwa mwezi huu especially wiki hii sitaweza kukugomboa popote, utaosha vyombo utie akili, uache umelo 🤣
 
Ukiingia kwenye restaurant usiposikia sauti ya bodaboda inapita kwa nje...
Hapo kimbia speed zooote
 
Back
Top Bottom